Eti haya maswali majibu yake ni nini?

hayo maswali ni mtego tu kwa kwa jinsi nionavyo!anakuwa anajaribu tu uone namna gani anavyojisikia kwako lakini lengo kubwa ni kubanjuka na wewe tu ingawa upo kwenye ndoa!

Ha ha ha kazi kweli kweli
 
Kweli huyo mtu anayesema hivyo how sure he is kuwa huyo hawara akiingia ndani hatakuwa na kasoro anazoziona kwa wife?

Ni lugha za mihemko tu; wakati mwingine hata si mihemko per se ila wanaume wazoefu a.k.a. bad boys, know exactly what, when and how to say; ndo maana wanawapanga wanawake.

 
Nimependa hapo nilipopigia mstari "kwa kipindi hicho". Maana watu wa hivyo wana mapenzi ya msimu; hata huyo anayempa maneno kama hayo in few years time anaonekana si mali kitu anaenda kuwaimbisha wengine same song; "ningekuwa sijaoa/olewa ningekuoa/olewa na wewe"

 
kuna ubaya?
 
Dena,haya ni mambo ya kawaida kwenye malavidavi,ni katika kushadadia tu.
 
You know what Cantalisia? I like you already!

Wanawake wengi hatuna uwezo wa ku analyse maneno ya wanaume. Mwanaume yeyote anaye speak dirty kuhusu mke au girlfriend wake unapaswa umkatae kwani he will do the same to you; ni tabia yake. Gentlemen hawawaongelei wanwake wao vibaya no matter what.

Mfano when I met my hubby the only thing alichonambia ni jina la ex wake baada ya kumuuliza; na hakunipa details why they broke up. Ni mimi ndiye niliyefanya research na kugundua kuwa the lady got married and lots of stories that he was cheating on him.

Hiyo ilinifanya nimpe credit.


Even the boyfriend before my hubby hakuwahi kumbonda ex wake kwangu; Na nina imani hata mimi hatakuwa alinisema vibaya kwa alonaye sasa kwa kuwa si tabia yake. hence I still believe wanaume wengi wana respect wanawake.

Wanaume wenye tabia mbovu strategy zao za kupata wasichana ni kubwabwaja; ooh demu alikuwa kicheche; ooh wala alikuwa anifikishi popote; ooh alikuwa ananiganda sikuwa na mpango nae; ukiona mwanume mwenye MDOMO KAMA CHUCHUNGE KIMBIA Faster! He is not a man enough! Hizo ni tabia za vivulana a.k.a sharobaro.


Sasa mwingine akiambiwa ningekuwa sijaoa ningekuoa wewe basi bichwa linakuwa kuubwa ndo kwanza anaendelea kuuliza "kwani mkeo ana kasoro gani?" huku full tabasamu. Ohh hajuhi kupika; hajuhi kusex; wewe ndio chagua; huku anakuja kwako kwa wizi. Kama ni chaguo amewekewa msumari kwa nini asifanye maamuzi magumu ya kukuchukua jumla?

 
aisee, hizo kauli huwa sipendi kuzisikia maana najua ni za uongo.
sipendi mwanaume anayemponda mwanamke mbele yangu.
sipendi mwanaume anayemlinganisha uzuri mpenzi wake na wanawake wengine.
sipendi wanaume wanaopenda kusifia viungo vya mwili hasa wakati wanaapproach.
sipendi wanaume wanaohadithia mapungufu ya wapenzi wao kwa watu wa nje.
hizo zote kauli. wanaume mjirekebishe.
 
na wanawake wanaotutangaza kuwa tuna 'vibamia' na bata afadhali tukiingia tunatapika hapo hapo?
 
na wanawake wanaotutangaza kuwa tuna 'vibamia' na bata afadhali tukiingia tunatapika hapo hapo?

hao wanawake wa wapi? wanaume ndio zenu kupondea mnapotoka kwa lengo la kusafisha mnapoenda. kwa mdada mwenye akili zake hawezi kufurahia hilo.
 
Hapo chacha; utasikia aisee umeumbika mguu mguu; macho macho; Sasa wenye miguu na macho mazuri humu duniani (hasa TZ) ni wangapi? Ntakuwaje na uhakika ukiona mwenye mguu na macho kama yangu hutamtamani? Kwa kweli hizo ni lugha za wanaume players.

 
Hapo chacha; utasikia aisee umeumbika mguu mguu; macho macho; Sasa wenye miguu na macho mazuri humu duniani (hasa TZ) ni wangapi? Ntakuwaje na uhakika ukiona mwenye mguu na macho kama yangu hutamtamani? Kwa kweli hizo ni lugha za wanaume players.

umeona eeeeh? wanawake wawe makini tu kwa kweli. ngoja niandae darasa tuongee mambo flani flani maana hii minjemba imezidi.
 
hizo ni lugha tu za kimihemko dada
watu wakiwa kwenye mihemko akili na mdomo havifanyi kazi kwa ushirikiano

umenikumbusha jamaa mmoja tunafanya nae kazi, maana huwa anasema kuwa akili ikiwa inafanya kazi mihemko na vitu vinavyohusiana hivyo vya kutamani ku do huwa havipo kabisa na pale inapofika wakati mtu anahitaji au kahemka akili huwa iko likizo kiidogo! hivyo nahisi mtu akisema hivyo huwa mind inafanyakazi anticlockwise kwani tayari anakuwa kahemka! Nahisi pia huyu mtu anakuwa na tamaa sana na kuona aliyenaye hamfai pale anapomuona mdada mrembo au hakuingia kwenye ndoa kwa shinikizo hivyo anakuwa anajuta kuwa nae!
 
nyumba kubwa na zawadi yako ya juice mpenzi umesema ukweli kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…