Eti haya maswali majibu yake ni nini?

Eti haya maswali majibu yake ni nini?

Habari zenu wapendwa wote wa jukwaa letu pendwa la MMU.

Natumaini wote muwazima kabisa na ni buheri wa afya japokuwa ya kwangu si njema sana ila nashukuru nimeweza hata kuandika haya.

Nimekuwa nikisikia nikikutana na watu mbalimbali wakisema " Ningekuwa sijaoa ningekuoa wewe"

AU "Ningekuwa sijaolewa ningeolewa na wewe" Nimejaribu kuzitafakari hizi kauli nimekosa majibu hebu waungwana na wataalamu hebu nisaidieni?

Unaoa au kuolewa kwa lazima mpaka ufikie kusema maneno kama hayo???

Au nitamaa tu ndo zinasumbua? Ama ni nini hasa?? Hebu nisaidieni

Nawatakia maandalizi mema ya weekend.

DA

Ukikutana na wa hivi mtoe "BARU" akienda kwingine atasema hayo hayo!
 
Nyumba kubwa aksante dada! Salute.
Kama sio juhudi zenu humu MMU, mapenzi ningeyaelewa lini na wapi MJ1 mie!
 
aisee, hizo kauli huwa sipendi kuzisikia maana najua ni za uongo.
sipendi mwanaume anayemponda mwanamke mbele yangu.
sipendi mwanaume anayemlinganisha uzuri mpenzi wake na wanawake wengine.
sipendi wanaume wanaopenda kusifia viungo vya mwili hasa wakati wanaapproach.
sipendi wanaume wanaohadithia mapungufu ya wapenzi wao kwa watu wa nje.
hizo zote kauli. wanaume mjirekebishe.

Ha ha hizo ni tabia chafu zote HAZIFAI
 
DA naomba nikunyooshee kuwa tamaa tu ndiyo inayowasumbua watu wa dizaini hiyo. Hivi ukimtongoza mtu mpaka umdanganye ndiyo akukubali? Inaeleweka kuwa inaweza kutokea kutokuelewana ndani ya nyumba lakini siyo kufikia kusema ulikosea kufanya uchaguzi. Mimi nadhani kama unataka kazi za nje fanya lakini siyo kwa kumkandia mkeo/girl friend wako vinginevyo muache umuoe huyo unayeona anakuvutia kwa kipindi hicho.

We Mzee wa Rula usitudanganye wenzio hakuna demu uliyempata bila kumdanganya kidogo, labda kama alijileta mwenyewe...
 
Nataka nije nioe bubu,nahs hataniambia maneno hayo,na wala kutakua hamna kelele.
 
Back
Top Bottom