Eti inawezekana?...UVUMILIVU MPAKA LINI?

Babu nitakutafuta nikwambie ni vitu gani niliomba serious kwa mungu na akanifanyia vile nitakavyo vingine hata sistahili kuwa navyo, acha kabisa na utachoka kabisa siku hiyo. Tatizo watu wanaomba bila imani

Sikatai kwamba ukiomba hujibiwi, lakini je ni vyote?.......Kila ulichoomba tangu uzaliwe ulikipata? Vingine naamini hujavipata...to be frank.

sasa itakuwaje hili la kuomba uvumilivu ujiaminishe kuwa lazima ukubaliwe? Usipokubaliwa hutachakachua?
 
DENA ndio maana nakupenda tungekuwa tunaambiana ukweli na matatizo yangepungua.

Mbona mnakubali ukweli wa upande mmoja tu jama? asi hata shilingi ina pande mbili au
 
Sikatai kwamba ukiomba hujibiwi, lakini je ni vyote?.......Kila ulichoomba tangu uzaliwe ulikipata? Vingine naamini hujavipata...to be frank.

sasa itakuwaje hili la kuomba uvumilivu ujiaminishe kuwa lazima ukubaliwe? Usipokubaliwa hutachakachua?

Bahati nzuri uvumilivu wa hiyo makitu nimezaliwa nao, nimekua nao na naendelea nao kama naweza sasa sidhani ukinioa oup sorry mwe nikiolewa nitashindwa
 
DENA ndio maana nakupenda tungekuwa tunaambiana ukweli na matatizo yangepungua.

Kabisa.

Ila kuna mdada mmoja bana mimi alinisimulia (Mie sina ujasiri huo) eti alikuwa kaolewa
lakini alikuwa dah hatulii jamaa akitoka kwenda kazini yeye mtindo mmoja anarudi kabla
hajatoka sasa hana kumbukumbu vizuri wakipiga story anasahau anasema kama leo nilipokuwa
ubungo nimeona hiki mara kile jamaa anamuuliza mbona hukuniambia kama unatoka anamwambia
nilikwenda kunanihii ila aaa jamaa mwenyewe kanichafua tu na kabamia kake na jamaa anafurahi
kuambiwa ukweli kama huo NILICHOKA na hawagombani ng'o kisa mdada kasema ukweli so ukweli
saa nyingine unasaidia my dear. Hii ni kweli kabisa wala si utani
 
Bahati nzuri uvumilivu wa hiyo makitu nimezaliwa nao, nimekua nao na naendelea nao kama naweza sasa sidhani ukinioa oup sorry mwe nikiolewa nitashindwa

Huyo ni Maty aliyezaliwa na uvumilivu, je ambao hawajazaliwa nao?
 
Maty bwana umeamua kunihukumu sasa haya bana nitajifunza kuwa mvumilivu dear usijali pole kama nimekukwaza
 
Babu sasa fanya analysis, nafikiri data unazo za kutosha; then ubandike matokeo!
 
Huyo mwanaume sijui katokea sayari gani
 
ooooops !
 
CPU kula tano.....you have made my day brighter kwa kucheka kimoyomoyo maana hawa wakoloni zangu wasijenimind bure.
 
Kumpenda Mungu ni pamoja na kuzishika sheria zake!!
Sio kuosha kikombe kwa nje wakati kwa ndani ni kichafu. Nikukubali udhaifu wako na kumuomba Mungu akupe neema ya kushinda. Nikuikana nafsi na kuacha kumsaidia shetani kazi zake, manake yeye ndio baba wa uovu wote.

Kusali tu haitushi, wala kujifariji ni na nani asiyetenda dhambi haitoshi kukufanya wewe u justify uovu. Kuhusu kujibiwa kwa maombi, Mungu anajibu kwa wakati wake na sio lazima ajibu kama unavyotaka wewe!!

Anakupa kile anachoona ni saizi yako, na kile ambacho utampa Mungu utukufu kwa kuwa nacho.

Sio kweli kwamba hatujui kama tunamkosea Mungu tufanyapo uovu ila tunajitaidi kujihesabia haki, wala hatufanyi toba ya kweli juu ya uovu tuutendao. Tumeshajihalalishia na wala hatutaki kubadilika tunasema haiwezekani. Je ni kweli haiwezekana???

Inawezekana kwa Neema ya Mungu!!!
 
Maty bwana umeamua kunihukumu sasa haya bana nitajifunza kuwa mvumilivu dear usijali pole kama nimekukwaza

Sijakuhukumu mpenzi wangu na wala hujanikwaza kabisa hapa tunaongelea pande mbili my dia. Kuna mtu aliwahi sema wakikutana wajuanao wanasapotiana kila kitu hapana sometimes lazima tupingane ili maisha yaendelee vyema. Hakuna alienikwaza hata kidogo kila mtu ana haki ya kuchangia aonacho ni sawa ni mijadala tu hapa mpenzi hakuna kingine
 
Huyo ni Maty aliyezaliwa na uvumilivu, je ambao hawajazaliwa nao?

babu msikilize mjukuu wako hapa chini hakuna kitu kinachoshindikana ukiamua mimi nilizaliwa na hasira za kihehe usipime tena nadhani zingine nilirithishwa zisizo zangu aseeeeee nilikaa chini nikamuomba mungu mpaka zinakaribia kuisha kabisa sasa. Hakuna kinachoshindikana kwa mungu ni kuamua tu na kusubiri

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…