kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Kuna ile kamati ya tenda wasijifanye eti ni malaika watu wawaamini tu. Tenda sio jambo la kushindanishwa tu mwenye bei ya chini eti anapewa.
Kuna umuhimu wa kamati kufanya utafiti sokoni ili kujua gharama halisi ya mradi wanaotangaza. Wakijidai wanaangalia nani mwenye bei ndogo wananchi watakuja na bei halisi toka sokoni.
Suala la rufaa baada ya tenda kutolewa sio suala la kuwatisha wakandarasi eti wasifanye watachelewesha mradi.
Lazima tuwe na utamaduni ambapo bei halisi sokoni ndio ziwe msingi kutoa tenda. Kama waombaji wote wataonekana wako nje kabisa ya bei sahihi sio eti yule wa chini anapewa tu.
Kinachotakiwa ni kuifuta hiyo tenda na kutangaza upya. Sio kampuni inapewa tu kwa kua wana quotation ya chini kuliko wengine.
Tumeona hapa juzi mombasa wanapewa kukarabati chombo kwa gharama karibu na ile ya kununulia chombo hicho kiliponunuliwa kipya.