Eti kufanya Engine Overhaul kunaondoa engine katika ubora na ufanisi daima?

Brother japo nitakuwa out of topic kidogo. Mm nahitaji kujua kwa bajaji inawezekana ukazifanyia overhaul zikarudi kwenye ubora ule ule na makadirio ya costs zinaweza kuwa kiasi gani?
 
Hizo engine ndogo ndogo achana na tabia ya kufanya overhaul nunua tu ingine japo unaweza ukanunua ingine nayo inaweza kuwa inakula oil, cha muhimu unanunua wapi.

Kuna engine za kufanya overhaul mfano za fuso kupanda huko unakuta engine mpya 16mil na overhaul 5mil sasa engine ya 1.2m overhaul ya nini. Ni mtazamo lakini.
 
Brother japo nitakuwa out of topic kidogo. Mm nahitaji kujua kwa bajaji inawezekana ukazifanyia overhaul zikarudi kwenye ubora ule ule na makadirio ya costs zinaweza kuwa kiasi gani?
Engine yoyote ile inafanyiwa overhaul.. kuhusu kiasi hapo ndio sina uhakika.

Ila kitu cha kuzingatia ni

1- FUNDI mzuri (Hapa ukikosea tu huna chako)

2- SPARE PARTS Original... (Usiweke ubahili)
 
Mkuu naomba kuuliza,kwa uzoefu wako engine ya 3sge ni kweli haiwezekani kufanyiwa overhaul ndio hizo engine kununua mswaki au mpya pale ilala ni ghali mno kuzizidi hata 4gr?
 
Niliwahi fanyia overhaul 2sz engine, mapicha niliyoyaona gari ilikua inalia kama trekta, oil inapungua, kumrudishia fundi akapaka maker meengi. ilikuja nizimikia mataa ya kamata. Best option ni kung'oa iliyopo na kuweka mswaki.
Nilikuona mkuu
 
Kuhusu engine mswaki... kuna kitu huwa sielewi...

Nitahakikishaje quality ya engine? Nitatambuaje kilomita ilizotembea?

-Kaveli-
 
Kuhusu engine mswaki... kuna kitu huwa sielewi...

Nitahakikishaje quality ya engine? Nitatambuaje kilomita ilizotembea?

-Kaveli-
tatizo huanzia utajauje km ilizotembea, niliwa kununua engine complete (1MZ) pale ilala na nikauliza nitajuaje uzee wa hii engine? nikajibiwa ni ngumu kujua. nikaichukua na kuifunga kwa imani. gari ilitulia kwa kipindi chote nilichokuwa kuwa nayo (3yrs) mpaka nikaiuza..
 
Kuhusu engine mswaki... kuna kitu huwa sielewi...

Nitahakikishaje quality ya engine? Nitatambuaje kilomita ilizotembea?

-Kaveli-
daaah aisee hilo swali huwa najiuliza sana mpaka huwa naona kama ni bora uagize mwenyewe engine ukiwa unajua na milage yake
 
Nenda Royal Motors Garage pale ubungo extenal opposite na geti la Nimr...

Hio garege Toyota tz na Nissan wenyewe wanapelekaga pale kaze zao wanazoshindwa... izo overhaul wanazifanya gari inarudi na nguvu ile ile ka ilivyokua mpya...

Mi na jamaa yangu sahidi tushapeleka magari yetu sku hizi tunapeta tuu garage service tuu
 
Du! Shida ni kwamba mimi niko mikoani, Mwanza kabisa.
 
Du! Shida ni kwamba mimi niko mikoani, Mwanza kabisa.
 
Nunua engine tu, overhaul miyeyusho. Mafundi wa bongo hawawezi kufanya overhaul vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…