-Angalia gharama.
-1NZ ni alumminium block. Ukipata fundi mzuri wa overhaul hilo tatizo litaondoka, ila mlio hautarudi kama ulivyokua, utaongezeka. Na asije mtu akakuambia vifaa vilivyowekwa na fundi wako ni feki ukaifungua tena, hapo ndio utakua umeiua kabisa.
Alminiam ni nyepesi, hivyo unapofunga zile bolt silinda head-block huwa hazikazi kama awali, ukisema uzifungue tena, ukifunga ndio zinapwerepweta kabisaaa na hapo ndipo oili italiwa.
Pia 1NZ engine maisha yake ni kilomita laki mmbili (200,000,km)life spane. Ikifika km 150,000 majanga yataanza kama kula oil, ku vibrate, kutoa mlio wa kugonga nk, hapo utabadili hadi taimingchain na tanshiner yake, gasket karibu zote, rings, kisha itaishi kwa km 50,000. Hapo utoe engine. Sasa angalia gari yako ina km ngapi.