Eti Makamba nae ameshtushwa na utitiri wa vituo vipya vya mafuta! Adai hana majibu

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Waziri wa Nishati, January Makamba ameshtushwa na utitiri wa vituo vipya vya mafuta vinavyojengwa nchini huku akiwaomba NEMC na Ewura taarifa imekuaje?

Kama Waziri mwenye dhamana hana majibu tukamuulize nani? Vituo vimeanza kujengwa mpaka vimemalizika na vinafanya kazi hadi leo hajui kwanini! Bei nzuri na ruzuku juu kwanini wafanyabiashara wasihamie huko wakiwemo wanasiasa?

Kwanini hawa wanasiasa wanapenda kutucheza shere! Faida kubwa kwa gharama ya hela za watanzania.

Your browser is not able to display this video.
 

Kituo kingine kimejengwa kabisa barabarani pale Stopover Kimara! Halafu mjinga mmoja anasema hajui hahahaha halafu na yeye ni waziri wa nishati hahahahaha
 
Wakaangalie flow meter huko Bandarini iko sawa?!!
 
Hivi mimi niulize,kuna ubaya gani wa kuwa na utitiro wa vituo vya mafuta?

Mbona kama hii Nchi ina watu wajinga Sana,kuna sheria wanavunja? Mbona hiyo ni biashara kama biashara zingine?

Eti utitiri,huu ni upumbavu,nilidhani watafutahia kwa sababu uchumi unakua na hapo wanapambana Ili kukidhi mahitaji ya mafuta..
 
Mshangae waziri wako anayeshangaa, idiots
 
Wanajenga sehemu haramu!
 
Na mimi nashauri hivyo, vituo vimezidi
Kuna kimoja kimejengwa Kawe pembeni ya kituo cha mabasi, yaani ni kaeneo kadogo na nyumba zimebanana sana.

Zikiingia daladala tatu hazienei, Lori kubwa la mafuta haliwezi kuingia, labda hayo mafuta watakuwa wanaleta na kirikuu.
 
Ni huduma kwa wananchi, acha vijengwe tu! Ila wajue magari ya kutumia gas na umeme yatakwamisha hiyo biashara.
 
Kazi kubwa ya vituo hivyo ni kutakatisha pesa chafu za wanasiasa wa chama tawala. Ukimjua mmiliki halisi wa Lake Oil utazimia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…