Kuna kimoja kimejengwa kawe pembeni ya kituo cha mabasi, yani ni kaeneo kadogo na nyumba zimebanana sana,
Zikiingia daladala tatu hazienei, Lori kubwa la mafuta haliwezi kuingia, labda hayo mafuta watakuwa wanaleta na kirikuu,
Waziri wa Nishati, January Makamba ameshtushwa na utitiri wa vituo vipya vya mafuta vinavyojengwa nchini huku akiwaomba NEMC na Ewura taarifa imekuaje?
Acha vituo vijengwe kwanza vinapendezesha mji kwani kwa standard kituo kikijengwa kunawekwa na supermarket
Sheria zilizopo hazitekelezeki kwani unapokuwa unataka mita 100 au 200 toka makazi ya watu kwa DSM haiwezekani.
Vituo vijengwe vijana wapate ajira wenye magari na wananchi wapate huduma na miji ipendeze. Ova