Eti mama anayenyonyesha anaweza beba mimba kama akikutana na mwanaume kimwili?

Eti mama anayenyonyesha anaweza beba mimba kama akikutana na mwanaume kimwili?

Mkuu usije tafuta mchawi wala nini mimi nilishakamatwa watoto wakapishana mwaka na miezi saba huwa inashtua lakini nikuleatu NO ABORTION
 
Kwa ufahamu wangu wa kibilojia,mama anayenyonyesha aweza pata mimba kwani hapo ni kazi ya vichocheo ama homone.Anaponyonyesha kuanzia mwezi wa pili mzunguko wa hormone(by negative feedback) unaruhusu yai kukomaa na hivyo likitoka laweza rutubishwa mara moja.
Kwa hiyo mkuu chukua hatua kwa faida ya mama,mtt na aliyetungwa kama tayari.
 
Poa mkuu!
 
umesha mbemenda mtoto ra sivyo mwambie asiendelee kumnyonyesha.......

Hakuna kitu kama kubemenda mtoto, kinachotakiwa hapo ni mama kupata lishe bora ili atengeneze maiziwa ya kutosha. Kumnyonyesha mtoto ilihali mama akiwa mjamzito kwa hatua za mwanzo haina madhara yeyote. Mama anashauriwa kuwa msafi hasa mara baada ya tendo la ndoa, ajisafishe vyema matiti na chuchu zake kabla hajamnyonyesha mtoto. Pia atatakiwa kusitisha kumnyonyesha huyo mwana, mimba ifikiapo umri wa kuanzia miezi sita, ili mwili uanze kutengeneza maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto ajaye. Mie sio daktari ila niliupata ushauri huo nilipomtembelea mtaalamu wa masuala ya uzazi, na nilimuuliza maswali ya kutosha. Na pia nimekuwa na rafiki zangu ambao walinyonyesha katika kipindi cha ujauzito na hawakuwaathiri watoto wao.
 
Nenda kiliniki ya Afya ya Mamam na Mtoto iliyo karibu yako (kiliniki uliyokuwa unahudhuria ukiwa mjamzito au nyingine) utapata maelezo mazuri na stadi za uzazi wa mpango bila malipo, ana kwa ana utapata wasaa wa kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa papo.
 
Back
Top Bottom