kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Nini maana ya marekani kusema wanakubali falsafa ya Samia. Kwa wale wanamapinduzi ndani ya chama cha mapinduzi na nchini kwa jumla maana yake jeuri ya tanzania kutaka kujitegemea na kujenga usawa kwa wananchi wake samia amemaliza. Siku hizi husikii tena uwekezaji mkubwa wa viwanda wala husikii tena nini kinaendelea kwenye serikali kudhibiti madini. Unachosikia ni kutiliana mikataba kukopa benki ya dunia au IMF huku kila wakitia sahihi kukopa wao binafsi wananeemeka maana benki ya dunia ni benki tu ya biashara yenye wanahisa wakubwa kutoka nchi za kibepari za magharibi.
Huko palestina tumeona jinsi marekani kupitia wakala wake Israel wanawachinja na kuangamiza taifa la Palestina. Hata neno moja kulaani toka tanzania hatujasikia. Miradi ya mipya ni ya upigaji tu. Kukopa benki ya dunia eti kuanzisha kampasi ya udom njombe ndio kitu gani wakati capacity ya majengo iliyoko udom hata nusu pengine haijafikiwa. La msingi ni uwekezaji kwenye viwanda maana hata hao wahitimu wanaishia umachinga tu.
Na kuna hili eti kujenga meli ya wokozi ziwa viktoria. Ukisikia utaona kama jambo muhimu ila linasukumwa na upigaji tu. Ukija kwenye umeme ni yaleyale matashi ya ubeberu yakifanikishwa na hiyo falsafa ya ubinafsi na uchoyo inayozalisha ufisadi inayoendelezwa na samia na kusifiwa na marekani. Nchi haitakiwi kujitosheleza umeme kwa kuhakikisha kuna uhaba au hujuma. Lengo hatutakiwi kua na umeme wa kutosha au wa bei rahisi ili nchi isiwe kivutio kwa wawekezaji. Yote hayo ni mipango ya mabeberu.
Lingine ni kutaka kuwapa wageni kuendesha miundombinu mikubwa kama reli na bandari mawasiliano na kadhalika kwa faida yao huku fedha ya umma mabilioni zimetumika kuijenga kwa lengo la kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa umma. Yaani umma kupitia serikali yao wawekeze kwenye SGR, bandari na kadhalika halafu wapewe wageni kuendesha huku wanaweka malengo yao na sio ya umma wa watanzania.
Ukisikia serikali ya nchi kama tanzania marekani wanasifia falsafa ya kiongozi wake ogopa kama ukoma. Ujue unawafaidisha wao na sera zao na sio nchi yako ukiacha vigogo wapigaji wanaofaidika binafsi.
Ifikapo 2025 twendeni kupata mzalendo kuongoza nchi kwa maendeleo ya umma kama jadi yetu. Vinginevyo tutaanza kujenga kwa kasi nchi ya majizi wachache yakidhibiti mali zote za taifa kisha amani tuliyozoea itatoweka.