Eti, mifuko ya plastiki marufuku!

Eti, mifuko ya plastiki marufuku!

Hakuna anayejali

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2023
Posts
418
Reaction score
526
Hakuna cha kuzuiwa ila ni mabadiliko ya aina ya mifuko. Nenda sokoni kanunuwe mboga, mihogo utapewa mfuko wa plastiki, chumvi zipo kwenye mifuko ya plastiki mi nadhani yalikuwa maamuzi ya kukurupuka tu.
 
Hakuna cha kuzuiwa ila ni mabadiliko ya aina ya mifuko.Nenda sokoni kanunuwe mboga,mihogo utapewa mfuko wa plastiki,chumvi zipo kwenye mifuko ya plastiki mi nadhani yalikuwa maamuzi ya kukurupuka tu.
Wapige marufuku na mawigi, rasta, pedi za wakubwa na za watoto na kondom
Hivi vitu vinachafua sana mazingira!
 
Wameibadilisha jina wanaiita vifungashio, ila walichofanya wazui plastiki(mifuko) walifanya jambo zuri sana。
 
Hakuna cha kuzuiwa ila ni mabadiliko ya aina ya mifuko.Nenda sokoni kanunuwe mboga,mihogo utapewa mfuko wa plastiki,chumvi zipo kwenye mifuko ya plastiki mi nadhani yalikuwa maamuzi ya kukurupuka tu.
Kabla ya kuandika tafiti ujue unachotaka kukiandika.
Hawajakataza mifuko yote ya plastiki, kabla ya kukataza walitoa viwango vya unene wa hizo plastiki.
Soko la Mbagala Rangitatu wslikuwepo watengenezaji wa hiyo mifuko iliyopigwa marufuku, mamlaka husika iliwakamata wote na kuchukua mashine zao za kutengeneza hiyo mifuko, hivi sasa haipo na wauza maji ya kandoro hawapo tena.
 
Hakuna cha kuzuiwa ila ni mabadiliko ya aina ya mifuko.Nenda sokoni kanunuwe mboga,mihogo utapewa mfuko wa plastiki,chumvi zipo kwenye mifuko ya plastiki mi nadhani yalikuwa maamuzi ya kukurupuka tu.
Unalialia wewe ukiwa wapi?
 
Hakuna cha kuzuiwa ila ni mabadiliko ya aina ya mifuko. Nenda sokoni kanunuwe mboga, mihogo utapewa mfuko wa plastiki, chumvi zipo kwenye mifuko ya plastiki mi nadhani yalikuwa maamuzi ya kukurupuka tu.
Kwani ilipigwa marufuku mifuko aina zote?
 
Nemc wameshafeli plus wizara ya mazingira,pumzi wamekata rusha wamepewa na wafanyabishara wa viwanda vya mifuko ya nylon
 
Hakuna cha kuzuiwa ila ni mabadiliko ya aina ya mifuko. Nenda sokoni kanunuwe mboga, mihogo utapewa mfuko wa plastiki, chumvi zipo kwenye mifuko ya plastiki mi nadhani yalikuwa maamuzi ya kukurupuka tu.
nasikitika kusema huna akili......
 
Ila vile vimfuko vyeusi hapana vilikua too much, bora vilipigwa marufuku....

Na huu upepo wa june basi unatembea zako kwa maringo kimfuko kinapepea kinakuja kukuvaa kichwani.
nakumbuka nilishaishi nyumba moja na muinjilist jamaa alikua chenga sana siku moja usiku upepo umeleta ule mfuki mweusi basi nimeenda kukojoa nje nikauokota nikaweka kwenye dust bin .....
badae ngoma 8 hivi paka wakafurumusha dude la uchafu mifuko kadhaa ikawa nje upepo ukipiga mfuko ukawa unazunguka kwenye mlango wa jamaa asee ilipigwa maombi hapo ndani sio mchezo
akipiga maombi kuna muda upepo unatulia anasifu asante yesu umemshinda shetani😂😂😂😂😂😂
akikaa kidogo upepo unaanza tena aloo maombi yanaanza upya nilicheka sana usiku huo.

asubuhi jamaa anawaelezea majirani eti katumiwa jini kalipiga na moto wa yesu hapo ndipo alinivunja mbavu maana angejua ni mfuko sijui angejisikiaje na mimi nikapiga kimya sikutia neno😂😂😂
 
Back
Top Bottom