nakumbuka nilishaishi nyumba moja na muinjilist jamaa alikua chenga sana siku moja usiku upepo umeleta ule mfuki mweusi basi nimeenda kukojoa nje nikauokota nikaweka kwenye dust bin .....
badae ngoma 8 hivi paka wakafurumusha dude la uchafu mifuko kadhaa ikawa nje upepo ukipiga mfuko ukawa unazunguka kwenye mlango wa jamaa asee ilipigwa maombi hapo ndani sio mchezo
akipiga maombi kuna muda upepo unatulia anasifu asante yesu umemshinda shetani😂😂😂😂😂😂
akikaa kidogo upepo unaanza tena aloo maombi yanaanza upya nilicheka sana usiku huo.
asubuhi jamaa anawaelezea majirani eti katumiwa jini kalipiga na moto wa yesu hapo ndipo alinivunja mbavu maana angejua ni mfuko sijui angejisikiaje na mimi nikapiga kimya sikutia neno😂😂😂