Just for Argument Sake.....
Hivi kuna kitu kama mke asiye bora?
Na kama yupo ni nani ambaye anafaa amuoe huyo?
Na kama Mungu anatupenda wote sawa, kwanini anichagulie mimi mke mbaya na wewe akupe mzuri?
Na je Mke akiwa bora na katikati ya ndoa akawa mapepe na hapo ni nani wa kulaumiwa?
Na wewe kama sio bora, je unahitaji mke bora?, kwanini huyo mwanamke bora abebe mzigo wa wewe ambae sio bora?
Haya ni baadhi tu ya maswali kwa yeyote awezae kunijibu....
Asanteni
VOR, Binafsi ninavyoona hakuna mke mbaya wala mume mbaya. Kila binadamu ameumbwa kwa tabia yake, na namna yake sijui niseme na Hulka yake.
Mume/mke anaweza akawa mbaya kwa huyu kumbe angeliishi na mwingine wangeendana tu vizuri.
Apart from hizi tabia nyingine mbaya kama uzinzi, ulevi nk nk, lakini tabia nyingine tunazo tumejikuta tu tunazo, mfano hasira,uchoyo,nk nk. Sasa kuna mtu anaweza akachukuliana na hasira alizonzoa mtu lakini mwingine hawezi, kuna mwingine anaweza akachukuliana na mtu mchafu, rafu rafu mwingine hawezi. Kuna mtu anaweza akachukuliana na mtu mlevi mwingine hawezi.
Tukumbuke kila mwanadamu ana udhaifu wake, JE mimi naweza kuchukuliana na udhaifu wa mwenzangu. Kama nikiweza tunaishi bila mikwaruzo, ukiniudhi najua jinsi ya kukueleza tunamaliza, nikikosea unajua kunirekebisha na ninakuelewa. Lakini kama huwezi kunielewa, na mimi sikuelewi huyu sio mke/mume mwema kwako, maisha yatakuwa ya ubishi na visasi kila siku.
Ndio maana sasa tunatakiwa kumuomba Mungu kwa bidii ili atukutanishe na yule ambaye mnaendana.
Na huyu ni Mungu pekee anaweza kwa sababu wengi tunaingia kwene ndoa sio kwa sababu nimeona naweza kuishi na huyu mtu na tukaenda sawasawa, ila wakati mwingine tunasukumwa tu na vitu vya nje kama vile uzuri, fedha, elimu, haja ya kuoa/kuoa nk nk nk.
Hebu jaribu kufikiria wewe ni mume wangu ukapatwa na hasira juu ya jambo fulani halafu ukaona njia sahihi ni kumuua huyo aliyekukosea, ukaniambia mimi kama mkeo nikakuambia twende tukamuue kabisa mume wangu na Rungu hili hapa, hivi nitakuwa msaidizi mzuri ktk hili kweli. Natakiwa nijue jinsi ya kuishusha hasira yako, kukupunguzia mastress badala ya kuyaongeza nk nk.
Mke/mume huyu ni mwema kwako????
Naishia hapo niko tayari kwa maswali zaidi.