Na bado, natamani hata mlipwe mshahara tarehe hamsini. Maprofessor na madokta wa vyuo vikuu wa siku hizi ni mzigo tu kwa jamii. Mkishalipwe mapesa na serikali basi mnaisaliti jamii iliyowasomesha, mnabaki kuisifia tu serikali na kujipendekeza ili mpate vyeo. Yaani ile value ya wana UDASA imepotea kabisa. Ndiyo maana hata serikali inaamua kuwafanyizia tu, maana hamna impact kwake. Ingekuwa ni UDASA ya akina Chachage na akina Haroub hapa najua pangechimbika. Lakini UDASA ya siku hizi ni label tu. Tangu Kikwete aanze kuteua mawaziri kutoka katikati ya wahadhiri, basi kila mmoja ni kujipendekeza tu, akidhani labda na yeye atateuliwa. Yaani nyie mcheleweshwe tu mshahara ikiwezekana mlipwe mwezi ujao, wasaliti wakubwa nyie.