Eti mpaka leo tarehe 37 serikali haijalipa mishahara taasisi zake nyingi mfano. vyuo vikuu!

mcfm40

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,452
Reaction score
3,151
Eti wanadai wanarekebisha mishahara ya zamani ili kuweza kulipa mishahara mipya. Sawali ni je hawakujua siku zote kwamba wanalipa mishahara mipya? Kinachoonekana ni kwamba serikali haina pesa. wanasubiri TRA wapeleke makusanyo. wanasingia kubadili mishahara ya zamani.
 
Mkuu bora umesema sababu manake jana nimekwenda bank kumenuna.....
 
ajabu sana.halafu yapo dodma yanatumbua kodi zetu huku serikali haina fedha za kuwalipa wafanyakazi!
 
NJI hiii wasiofanya kazi za maana (mfano waongo wanaojiita wanaSIHA-sa) ndio wanapewa kipaumbele kwenye kulipwa
 
Usihofu ikifika tarehe 43 itakua mmelipwa mishahara yote.
 
Njaa tupu huku mitaani. Ikifika wiki ijayo bila pesa, itakuwa balaa.
 

Na bado, natamani hata mlipwe mshahara tarehe hamsini. Maprofessor na madokta wa vyuo vikuu wa siku hizi ni mzigo tu kwa jamii. Mkishalipwe mapesa na serikali basi mnaisaliti jamii iliyowasomesha, mnabaki kuisifia tu serikali na kujipendekeza ili mpate vyeo. Yaani ile value ya wana UDASA imepotea kabisa. Ndiyo maana hata serikali inaamua kuwafanyizia tu, maana hamna impact kwake. Ingekuwa ni UDASA ya akina Chachage na akina Haroub hapa najua pangechimbika. Lakini UDASA ya siku hizi ni label tu. Tangu Kikwete aanze kuteua mawaziri kutoka katikati ya wahadhiri, basi kila mmoja ni kujipendekeza tu, akidhani labda na yeye atateuliwa. Yaani nyie mcheleweshwe tu mshahara ikiwezekana mlipwe mwezi ujao, wasaliti wakubwa nyie.
 
Sikujua kama tarehe inafika hadi 37
 
mishaharaaaa au poshooo???

ya wapi hiyoo? poleni mnooo
 
Mh mkuu hiyo tarehe 37 ni ya nchu gani? Anyway hii ndo serikali yetu sikivu
 
serikali ya huyu mheshimiwa hainaa helaaaaaa jamaa ana matumizi makubwa kuliko hela anayeingizaaaaa
 

Leo ni tarehe 39 mwezi wa serikali mkuu........sio tarehe 37
 
Usitudanganye bana, kipindi cha akina chachage licha ya mishahara kuchelewa bado ilikuwa kiduchu...mpaka chachage alipotunga kitabu chake cha makuadi wa soko huria akaigusia hiyo issue kiaina kwa kuonyesha taswira ya maprofesa wanamkimbiza mwizi wa nguruwe wao..
 

Usijali ndugu. Sisi wengine ni wanamageuzi wa ukweli! hilo la Udasa linashughulikiwa na tunafanya kazi kubwa kupambana na wasomi wanaojipendekeza kwa watawala. na muda sis muda udasa ya kweli itarejea. Lile la juzi ni jamaa mmoja wa CCM udasa mnamfaham alifanya vile. na wengi hawakugundua walikuja kujua baadaye. Uongozi wa udasa umeomba radhi!
 
Mnayomengi ya kuomba radhi...tena bado sana kujitambua...mmepeleka vijana field bila pesa, bila kuwatetea, na mnaenda kuwakagua kwa kuwaharass.... watoto wanadharirika mjini nyinyi kimya mko busy kuandaa mdahalo wa ccm.
 
isotope; Laiti ungejua kwamba hata hiyo mishahara mipya ameipigania Chachage wala usingesema. Watafute wanataaluma wenzako wakuambie. Siku tunamzika Chachage, Kikwete mwenyewe alisema kwamba Chachage alipigania mabadiliko ambayo hajayafaidi. Maana wakati mabadiliko ya mshahara wa malecturer ulipofanyika ndipo yeye alikufa. Hilo hata sisi wamachinga tunalijua kwamba kama siyo Chachage hiyo mishahara mnayolipwa, msingekuwa nayo. Chachage alikufa na UDASA wake, huo ndiyo ukweli. Mliobaki sasa hivi ni vimbelembele na viherehere kwa Kikwete kutafuta nafasi za kuteuliwa. Watu ambao miaka ya nyuma tulikuwa tunawategemea kwa kutoa hoja nzito nzito za kuichallenge serikali, sasa hivi mmekuwa wavivu wa kuchambua mambo kushinda hata wanafunzi wenu.
 
Last edited by a moderator:
Mnayomengi ya kuomba radhi...tena bado sana kujitambua...mmepeleka vijana field bila pesa, bila kuwatetea, na mnaenda kuwakagua kwa kuwaharass.... watoto wanadharirika mjini nyinyi kimya mko busy kuandaa mdahalo wa ccm.

Usijali kama una tatizo utamweleza mkaguzi wako atakuelewa. Ssis ni binadamu tunaelewa mazingira mliyonayo kwa sasa. Sasa wewe km unajua hujaweza kufanya field yako vizuri kwa sababu ya matatizo ya allowance kwa nini ukubali ukaguliwe! Mweleze mwalimu wako ukweli ili atakapokufanyia assessment alizingatie hilo. Halafu usiwe mbinafsi mdogo wangu, mdahalo pia ni jambo la muhimu kwa taifa ingawa ulivurugwa na watu wachache wenye malengo yao
 
Sawa, kuhusu Chachage naomba nisiongee mengi sina habari za kutosha..Naomba niongee juu ya kilichoiua UDASA. UDASA iliuliwa na Mkandala kupitia REDET... Udasa ilikuwa inategemea watu radical wa social science..Mkandala akawadaka na kuwanyenyekeza wato kupitia posho nono aliyokuwa akiwalipa kwenda kukusanya maoni au kufundisha chuo cha demokrasia zanzibar.. Kila mtu akawa hataoi maoni huru iliaweze kufaidi vya redet, hatimaye wote wamegeuka kuwa makada wa ccm, mzee bunsen burner akiwa mfano wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…