Eti Mtoto wa kiume unaangalia Tamthiliya ya Sultan

Eti Mtoto wa kiume unaangalia Tamthiliya ya Sultan

Hazchem plate

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Posts
11,048
Reaction score
15,465
Mtoto Wa kiume unakaa kitako kucheki huu upuuzi ili iweje?? Yaani unashindwa kucheki hata Prison Break unacheki huu Uchuro???

Ndio shida ya ujuaji, unaishia kuwa MJINGA DAIMA. Sultan imebase kwenye HISTORIA YA DOLA YA OTTOMAN. Kwa mtu unayependa KUJIFUNZA, huwezi kulinganisha SULTAN na upuuzi wa PRISON BREAK. Historia ya Uturuki kuitawala ULAYA, imesimuliwa humo tofauti na hayo maigizo ya kutoroka gerezani ambayo ni ya kutunga.

Kwa watalii na wengine tunaopenda kutembea, huwezi fika Uturuki halafu usitembelee maeneo ya kihistoria kama Ikulu ya Topkapi na Mji wa Instabul (Constantinople) kama utakuwa umeshawahi kuona Tamthilia ya Sultan. Hii ni sawa na kusoma kitabu, ni vile tumeumbwa na ubongo wa ajabu wa kutopenda kujua yaliyo mbali nasi.

Najua, kwa comment hii watainuka vichwa maji wengi kurusha upupu lkn kama taifa, tutambue kuwa FASIHI ni sehemu muhimu ya kuhuisha UBONGO. Nakumbuka miaka kadhaa nyuma kulikuwa na mashindano yanaitwa CELTEL AFRICA CHALLENGE ambapo vyuo vikuu mbali mbali vya Africa vilishindana na chuo bingwa kilipata top prize ya hadi $5m. Nasikitika, Tanzania ilikuwa kwenye viwango vile vile vinavyooneshwa na Taifa Stars. Kama Tanzanian intellectual anaulizwa Timbuktu Empire ilikuwa wapi na anapewa multiple choice na bado anakosa, kuna ujinga zaidi ya kutoangalia historical dramas enyi wazee wa madesa?

Ama kuhusu ushoga, Sumbulah ni jambo lingine lenye kuonesha UPUNGUFU WA UELEWA na mgomo tulionao kujifunza. Falme na Dola za Urithi za zamani, zilikuwa na taratibu za kuwa na MATOWASHI ambao ni wafanyakazi wa kiume kwenye women folk (harem) ya mfalme. Hawa, ili wasije kuwa na uhusiano wa kingono na malkia au masuria, huasiwa au kuondolewa kabisa uume...ndio kama Sumbulah Khaja...hii nayo ni elimu.

Tusijitie UJINGA tukauita UANAUME na ulimbukeni ukatutawala. Tamthilia kama Sultan(Turkish), Jumong na Jewellery In the Palace(Korean) zina nafasi kubwa ya kutumika kwa educational and heritage purposes kuliko prison break and the likes.

Kwako wewe ndugu yangu usiyependa ushoga, kama kweli wewe ni baba, jitathmini matumizi ya maneno kama COZ, BHANA, XAXA hatare n.k
 
Mtoto Wa kiume unakaa kitako kucheki huu upuuzi. Unatafuta Bwana?? Utaolewa boya ww Changamkaaaa. Unashindwa kucheki Hata Prison Break unacheki huu Uchuro???

Utaolewa Na Ndevu zako
We binti tunapangiana cha kuona
 
Back
Top Bottom