Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
Wanangu niaje?
Mi niko poa na Jumamosi ndio kama hii ishaibuka kudadadeki, kila ishu inanitaka mimi, ...dah...
Dah nimechelewa kuamka leo halafu dizaini halafu nilikuwa na mpango wa kuruka tauni fasta kuna mchongo wangu, ila ndio nikisema niibuke na daladala ndio nitakua nimezingua mazima.
Manake, mpaka nigombanie kwanza, nipate chansi watu watege mingo kituo kwa kituo, mpaka nifike tauni si jioni hiyo mwanangu?
Hapo si bora uwe na mkoko wako mwenyewe unaumiliki? Manake hapo ukipata mchongo tu fasta unaruka nini, ..fresh unakamilisha ukirudi unarekebisha mitikasi mingine.
Uongo mwanangu?
Mkoko ndio mpango mzima kwa yanki ambaye unaishi tauni, asikudanganye mtu kama kweli we mtu wa michongo ingawa masela wanawacheka sana mayanki wenzao wanapowaona wamechukua mkopo, halafu siku mbili tatu unamuona mwana anasukuma ndinga, halafu mtu mzima anaishi kwenye nyumba ya kupanga.
Huwa wanaonekana kama hawana akili watu dizaini hizi manake kwa mtazamo wa wana ambao wako kitaa ni kwamba ndinga inakuwa na mitikasi mingi kiasi kwamba itakusababishia ushindwe kupiga hatua nyingine za kimaendeleo, kwa sababu deile inakuwa inahitaji mkwanja ikae sawa.
Si unajua tena ndinga?
Mambo ya wese, mara kwenda kuipiga sopu, na hizi ishu kama za kupigwa pasi kitaa zinakuwa za kawaida tu kwa hiyo mambo ya gereji na fundi huwa yanakuja tu mara kwa mara.
Umeona?
Sasa hapo ndio unakuta mtu mzima hata ishu nyingine kama za kujipiga sopu mwenyewe, labda pamba, au kupiga jeki familia nini au hata watu wakikuibukia nini kutaka labda uwapige tafu kwa ishu flani unakuwa huna, na ukiwaambia huna ile kukutrasti moja kwa moja inakuwaga ngumu.
Unasukuma mkoko wa maana halafu huna kitu?
Ndio madongo yanapoanzia hapo kwamba labda mtu mzima bishoo, unamaindi kuonekana uko juu wakati huna lolote, kama vipi huo mkwanja wa ndunga si bora ungenunua mjengo ukalikita?
Kutokana na mdongo hayo mtu mzima nikaona kama vipi nifunguke, kweli kuna watu wanafuata mkumbo, dizaini wanabugi kwa kuiga baada ya kuona Zee linasukuma ndinga, anaona na yeye asukume ili wawe levo, lakini anasahau kwamba mwenzake alifikiria mambo kwanza kabla hajaamua ile moja kwa moja kuchukua mkoko.
Hizi ishu mjue zinaendana na mishemishe!
Kwa mtu wa michongo, kukimbilia usafiri ndio mpango, si mtu wa ishu? Hizi muvumenti unafikiri unazimalizaje kama huwezi kumuvu hia endi zea?
Ukisema uchukue mkebe mwanangu, unaweza kujikuta mkwanja wote unaumalizia kwenye mkebe manake jamaa nao wale ukimkodi kutoka hapa na pale tu utasikia mwekundu!
Sasa kama una misele siku nzima si ndio itakutaka kilo nzima kwa kushughulikia mchongo wa kilo na nusu? Halafu hii michongo wanangu ndio unaweza kujikuta unapiga mkwanja wa kuangusha mjengo na mambo mengine kama haya kwa hiyo mimi kama Zee...
. ..unanielewa lakini?
Mimi kama Zee naona bwana suala la mkoko kwa mtu na mitikasi yake naona kama ni bora uanze na mkoko ili kurahisisha michongo halafu mambo ya mjengo yatakuja tu na huu ni mtazamo wangu uinaweza lakini ukawa na wako pia.
Naweza kuwa najitetea!
Si unanijua na mie tena mambo zangu?
Ila kimsingi pa kulala muhimu lakini unawezaje kulala wakati huna mchongo?
Imejini yuaself, mi nasepa wiki ijayo kama vipi mwanangu au sio?
Wanlav