POTOSHI Eti Nchimbi amemwambia Rais Samia "Kama Mnataka Kunitimua, nitimueni leoleo

POTOSHI Eti Nchimbi amemwambia Rais Samia "Kama Mnataka Kunitimua, nitimueni leoleo

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
1778045164507.png
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na kipande cha video kinachosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kikimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Emmanuel Nchimbi akitamka kuwa kama wanataka kumtimua basi wamtimue.

Nchimbi anasikika akisema

"Na kuna mambo mengine ya msingi. Kuna wakati watu wanasema Nchimbi tatizo lake ana misimamo simamo hivi. Ni kweli, kwenye mambo ya msingi mimi nina msimamo. Na hili lazima tuelewane, ni jambo la kawaida tu. Kama mnataka kunitimua kwa msimamo, nitimueni leo leo. Kwenye mambo ya msingi lazima uwe na msimamo. Na ndiyo moja ya viapo vya chama chetu, mwana CCM mwenye msimamo ni dhumuni la pili tu, ndiyo sifa ya kuwa mwanachama. Nitasimulia hiyo mwaka 2000..."

Je, uhalisia ni upi?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa Dkt. Nchimbi aliyazungumza maneno hayo lakini hakuwa akimuambia Rais Samia kama inavyodaiwa bali aliyzungumza akiwa kwenye kutano wa hadhara kuwajibu watu wanazungumzia kuhusu misimamo yake.

Nchimi alizungumza maneno hayo muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama Chama cha mapinduzi January 2024, hivyo video hiyo imekuwepo mtandaoni kuanzia mwaka 2024.

Mathalani mtumiaji mmoja wa mtandao wa Youtube alichapisha video hiyo Januari 18, 2024 ikiambatana na ujumbe "HUYU NDIYE EMMANUEL NCHIMBI KATIBU MKUU CCM KAZINI". Tazama hapa

1777989136168-png.3584187
Wakurugenzi wana kura katika vikao vya NEC ya CCM?
Wao wanakusanya maduhuri, ni rahisi huyo mmoja kuwa na ukwasi kama wa marehemu Edo kumuwezesha kupata uungwaji mwingi mkono

As anatoa maagizo ya kutafutiwa hela ya safari ya matumaini part 2
 
Hii ni strategy, CCM wameshabaini kuwa hawakubaliki hivyo wanatengeneza mtu atakayeonekana kuwa hayuko sawa na hao mabazazi akina Samia. Style ileile waliyoitumia kuwaletea Mwendakuzimu Jiwe sasa wanawatengenezea mtu mwingine mtakayedhani kuwa yuko kinyume na establishment.
Be cautious.
Nakubaliana 100%

Nilishasema kama akubaliani nao kwanini asikae pembeni?
 
Fisiem ni Fisiem tu
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom