Sawa Mkuu, lakini vingine havijaumbwa bali vimetengezwa na binadamu kulingana na mazingira yao; kwa mfano ugali-wali ni vya kutengenezwa tu na binadamu na havifanani dunia nzima, ugali naopikwa Tanzania sio sawa na ugali unaopikwa Sweden, kuna siku rafiki yangu Mswidish aliniambia leo twende ukale ugali, nilikuwa nimekaa Sweden kwa muda wa miezi 6 na nimemiss kweli chakula cha nyumbani (Tz) hususani ugali na nyama choma. Basi akanipeleka kwenye mgahawa unaomilikiwa na mtu kutoka Botswana, kwa kuwa mmiliki wa mgahawa alikuwa kutoka Afrika, na rafiki yangu alishakuja Tz akala ugali na kuupenda, alijua moja kwa moja tukifika pale nikimweleza yule Mtswana atatupikia ugali mtama kama wa Tz. Basi akampigia simu, akamwambia tukipikie ugali tutakuja jioni kula, nakuja na ndugu yako kutoka Afrika. Huwezi kuamini, tulipofika tulikuta uji mzito wa kuchota na kijiko !!!! Ikabidi nimwombe niwapike ugali waone ukoje, basi wakaniandalia maji, nikayasimamia yakachemka kama huko kwetu, nikaweka unga na kuanza kupika kwa kuzungusha mwiko kama ambavyo ugali unapikwa, wao wanashangaa tu, wakabaki kupiga picha - still and mobile. Kwa kweli wote walipenda ugali ule, week'nd nyingine wakaniambia niende tena kuwafundisha, baada ya kumaliza shule na kurudi Tz mpaka sasa wananiambia wanapika ugali na wakisahau wanaangali picha walizonipiga !!!!