Eti, nikalale wapi?

Eti, nikalale wapi?

Ndiyo maana kameanza kunitingishia
d04b6172a1a3ff3ea06bf4f96df69822.jpg
 
Yaani ndio kama hivi, maana hata sielewielewi.

Saa mbili kamili usiku:

Bibi yenu: We mzee msosi tayari, nikutengenezee kachumbari?
Mimi: Tena weka pilipili ya kutosha mama, nina apetaiti ya watu wanne.
Bibi yenu: Haya baba, ole wako nishike mipilipili afu usile.
Mimi: Mama bhana.... umeanza lini kukosa imani na mimi??

Saa nne kamili usiku:

Bibi: We baba wewe, mbona huji? Mi nasinzia nataka nikalale.
Mimi: Ayaaa, nlisahau kukuambia leo kuna mechi... PSG Vs Barcelona. Siwezi kulala bila kumwona Messi akicheza
Bibi: Duh... we baba wewe. Kuna mpira kweli au michepuko?
mimi: mama huniamini? gugo soccernet.... najua hapo unaangalia movie huwezi weka channel ya mpira.
Bibi: Haya bhana, ila hii mipira yako hata siielewi.... Haina msimu?

Saa sita kamili usiku:

Bibi: We baba wewe.... mpira haujaisha? Mi nafunga geti naenda kulala
Mimi: Duh... mamito, rudishia tu geti nakuja fasta.
Bibi: Kasema nani? Bwana kama unachelewa kuja ulale hukohuko. Unaniudhi sana bhana..
Mimi: Mamito tuko wote hapa na kina Mtambuzi, Watu8 na Kaizer tunatafakari kwanini leo Messi hajafunga
Bibi: To hell na mampira yako. Ukichelewa dakika kumi nafunga geti... isije ukawa uko na yale unayojifanya marafiki zako ( Madame B na Evelyn Salt) afu unaniletea uchizi wako tu hapa...
Mimi: Hahahahaaa wewe bhana.... dakika tano ntakuwa nshafika hapo mbona??

Saa saba na robo:

Mimi: Washkaji, shemeji enu kawa mkali ngoja niwahi home
Kaizer: Hommie kumbe siku hizi mkeo anakutawala?
Mtambuzi: We babu ushawekewa limbwata
Mentor: Kama ndo hivyo mi sitaoa hakyamama
ray lee
: We babu kama ni hivyo Michelle baki naye mwenyewe
gorgeousmimi: babu usiwasikilize hawa muwahi bibi bhana
Apologise lady: Leo ndo ntajua kama ODM ni mwanaume. Nimetoka mbali kote huko afu uniache hapa.
Eshy m.s : nyoo, na mie nlietokea Arusha?
lara 1: Ahahaahaaa utajiju na mapouwddeeer
Mimi: Acheni ubweg.e.... Zenaaaa.... nipe bili yangu
Zena: Hahahahahaha leo unawahi home kama mchumba... nyooo... mxieuwww tarehe zimegombaaa
Mimi: We bwe.geee nini...... ongeza bia hapa watu wanywe.
Zena: Ningeshangaa
Meza:Bia, bia, bia, nyagi, zanzi, grants, amarula, black label.........
Glasi: kwah kwah... kroooooo...kwah kroooo

Saa nane:

Simu:ngrriiiiiiii......... MY WIFE. (duh!!)
Shetani: Piga chini hiyo. Zuga hujaisikia babu....
Mimi: Umenena vyema
Simu:Ngriiiiiii
Shetani: Babu fanya kama nlivokuambia, kwa manufaa ya ndoa yako. Achana na hiyo simu.
Mimi: Poa......Kimyaaaa

Saa tisa kamili:

Mimi: Oyaaaa.... angalieni bia yangu, toilet wapi?
Dena Amsi: wee nawe, washroom si kule? Pita kwa hapa hivi......
Mimi: Kona kushoto kulia kushoto kulia..... mara.... geti hili..... LOCKED.
Mimi: Chukua simu.... scrow... MY WIFE... Piga
SIMU: namba ya mteja unayempigia hapatikani kwa sasa, tafadhali jaribu tena baadaye.....
Mbwa: Wow wow wow.........
Mimi: Piga tena....Holaaaaa....Damn. Gonga geti holaaaa

Tisa na nusu:

Simu: Ngriiiiii ( miss chagga)
Mimi: Zima simu. Afanaaleki.... kufa hakuna breki!!! Hamnipati tena nyie walevi

Angalia muda hapo. Geti limefungwa, ntalala wapi???

Nimhukumu nani??

1. Marafiki?
2. Mpira?
3. Pombe?
4. Muda?


Nikalale wapi? (cheki muda nlioposti)
1. Kwa Zena Wa Kaunta?
2. Bar
3. Kwa swahiba
4. Getini niliwe na mbu??
5. Jibu A na B yote ni sawa

Wasalaam
ODM
Kaunta ya Juu
Boko Basihaya.

CC: sister, Heaven on Earth kwa maombi.
Dah....Ruka Ukuta huo...JKT ulienda kula maharage?[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Huu uzi duh......ila umeeditiwa kinyama na kiranja mkuu
 
Back
Top Bottom