suala si kuomba tu talaka lazima kuwe na sababu za kuomba hiyo talaka,kwanza lazima mwomba talaka aonyeshe kuwa ndoa yake haiwezekaniki tena hivo lazima aende baraza la usuluhishi hapo kama watashindwa kusuluhisha ndio aende mahakamani akipeleka petition yake,barua kutoka baraza la usuluhishi kuwa wameshindwa kuwasuluhisha, nakala ya cheti cha ndoa na vielelezo vinginevyo vitakavoambana na hiyo petition yake. KTk hiyo petition lazima aeleze ni vitu ghani vinamsukuma kuomba talaka kama mwenzake ni mwasherati usiovumilika manake kumfumania mtu siku moja tu sii sababu ya kuomba talaka lazima uonyeshe umeumizwa vipi na huo uasherati wake, au kama umeumizwa sana kwa kichapo cha mda mrefu(phyisical inujuries nk......pia mwomba talaka aweza kuambatanisha na orodha ya mali walizochuma pamoja na uthibitisho wake kama nakala z ahati ya nyumba magari nk ili kuomba mgawanyo wa mali, na pia idadi ya watoto aliowazaa na ambao angetaka kuwalea(custody of a child nk????)ktk kutoa talaka mahaka lazima ijiridhshe kwanza na ushahidi husika na pia ktk mgawo watoto ndo wanapewa first priority,,,custody itategema kipato na mazingira watakayoishi hao watoto nk nk ......nimechoka mwenye Marriage Act 1971 R.E 2002 atacheki,,,....JAMANI KABLA YA KUONA CHUNGUZANENI VEMA MANAKE TALAKA SII NJEMA SANA INAHARIBU FUTURE YA WATOTO NA WENGI WANAISHI KTK STRESS NK...