Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 221
- 542
Tunaposema Tanzania inahitaji viongozi wenye maono,malengo na uzalendo wa kweli tunamaanisha. Ni juzi tu train ya umeme imeanza kazi huku Stigler gorge ikiwa imeanza kuchangia kiasi cha megawatt kwenye gridi ya taifa ila cha kushangaza na kitia huzuni ni kwamba badala ya kuwa na mkakati mahususi wa kuhakikisha umeme haukatiki kwa namna yoyote Ile hata kwa ku dedicate megawatt kadhaa just for train peke yake, viongozi wanakuja na mkakati wa kinunua engine za Diesel eti kwajili ya kuendesha SGR pale umeme unapokatika.
Hakuna mpango wowote unaowekwa mezani kuhakikisha umeme haukatiki, mabilion ya pesa yamewekezwa kwenye umeme pamoja na train ya kisasa ila naona viongozi wameamua ku sabotage na kurudisha Tanzania kwenye giza.
Viongozi wetu unapowaona wanapita na magari ya kifahari na suti nzuri za kuvutia unawezawaona kama ni watu wa maana sana ila kiukweli ni tofauti na vile tunavyowaona, wengi ni less creative, wapenda rushwa na madaraka, uwezo mdogo katika kifikiri na kutenda, na wengi hufikiria zaidi matumbo yao kuliko maendeleo halisi ya nchi ya Tanzania.
Mama Samia angalia sana watu unawapa nafasi za kubeba maono na ndoto za watanzania, wengi wa hawa viongozi wanatulazimisha kuwa umasikini, na ujinga kuwa sehemu ya maisha yetu.
Train ya SGR imetupa sifa kubwa kama watanzania duniani kote ila hili la kununua engine za diesel badala ya kuimarisha upatikanaji wa umeme unaenda kutunyong'onyeza, kutubagaza, kituaibisha na kutufanya tuonekane kituko kwenye Dunia hii ya sayansi na teknologia.
Naomba Rais Samia uchunguze kwa makini huyu aliyeleta wazo la kununua engine za Diesel Ili kujua nani ana ratibu mambo haya ya kihuni na aseme ni nchi gani duniani iliyonunua train za umeme alafu wakaagiza tena engine za diesel kwajili ya kuendesha train ya umeme.
Ila pia msichukie sana wananchi wanavyomsifu JPM kwa namna alivokuwa anapambana kwa nia ya dhati ya kuiletea Tanzania maendeleo ya kweli na heshima duniani. JPM asinge tolerate mambo kama haya.