Eti Train ya Umeme kununuliwa engine za Diesel ⛽

Biashara za watu mkuu.
Diesel inalipa mkuu!
 
Kwakua sielewi treni ya SGR inavyofanya kazi hiki ninachoandika kisichukuliwe serious sana.

Badala ya engine haiwezekani kununua generators za kusupply umeme huu mwingine unapokata?

Au hiki hapa

Treni inatumia umeme. Umeme unakata treni haiendi.

Suluhu zipo mbili. Kujua kwanini umeme unakata na kutafuta suluhu au kununua engines za diesel. Ipi ni profitable in the long run?
 
Kwani mnaweza kuwa na majibu zaidi ya "Fake news" "Uzushi" "Upotoshaji" "Uchonganishi" ??.....Ufafanuzi uliotolewa jana usiku usiku mbona haukusema ni Fake news? 😲😮
Habari za kutunga ndio sifa ya ulimwengu wa sasa wa mitandao. Bahati mbaya zikikutana na wajinga wengi huchukuliwa ndio za kweli.
 
Fake tu, usitishwe na lugha ya kingereza, ndege za ATCL hazijaanza kwenda huko Ulaya, usafiri wa anga sio sawa na madaladala, kuna taratibu za mamlaka za anga kusaini kwanza mikataba ya kufanya biashara baina ya nchi zao na Tanzania,

Mkuu sekta ya anga sio nyepesi kama tunavyoongopeana huku mitaani.
 
Hii habari iko kwenye reliable sources nyingi tu sasa sijui wabisha nini.
Bora hata hiyo ya vichwa vya train. Hii habari ni reliable
 
Hii habari iko kwenye reliable sources nyingi tu sasa sijui wabisha nini.
Bora hata hiyo ya vichwa vya train. Hii habari ni reliable
Haiwezi kuwa reliable kwa sababu ATCL haijamaliza kuingia mikataba na mamlaka za anga za mataifa hayo ya Ulaya.

Usitishwe na kizungu hicho, ni habari za upotoshaji sawa na nyingine zozote.
 
Haiwezi kuwa reliable kwa sababu ATCL haijamaliza kuingia mikataba na mamlaka za anga za mataifa hayo ya Ulaya.

Usitishwe na kizungu hicho, ni habari za upotoshaji sawa na nyingine zozote.
Kweli mtu huamua kuamini anachokiamini. Unapingana na media outlets zinazohusika ana usafiri wa anga? Hapo wametoa list ikiwemo pakistan...
Kweli you only see what your eyes want to see.
Shida sio kiingereza, na ndiyo maana nimechambua links za kukutumia na ndo maana nimekutumia links za reliable sources na si any source
 
Tatizo ni dereva mwenyewe. Mimi Huwa namuona hamna kitu kabisa. Alifikaje hapo. Hana Nia nzur na nchi,Hana uwezo wa kuendesha gari, uwezo wake wa kujenga hoja na kuongea ni mdogo,haeleweki falsafa yake ya udereva ni ipi. Lakini Kuna wajinga utawasikia mitano tena. Huwezi ukawa na akili timamu ukampa mitano tena dereva wa hovyo kiasi hicho.
 
Hii habari ingekuwa ya kweli kuna mtu ningemdharau mpaka siku yake ya mwisho. Hata hivyo nafikiri kuna ukweli ndani yake ila wameona response ya public imekuwa negative sana wamaamua kukanusha.
 
Tanzania kuna nchi bado haijaweza kupeleka ndege zake, amini vyanzo vya ndani punguza huo utumwa wa kuamini kila kinachotoka huko nje. Punguza kujidharau.
 
Ununuzi wa vichwa vya diesel kwangu naona kama kiini macho. Kwa taarifa hii ni dhahiri kwamba Bwawa la Mwl. Nyerere limefeli tena mapema kweupe pamoja na majigambo yote ya serikali.
 
Habari za kutunga ndio sifa ya ulimwengu wa sasa wa mitandao. Bahati mbaya zikikutana na wajinga wengi huchukuliwa ndio za kweli.
Kumbe taarifa zote za treni kukwama mbugani kwa masaa kadhaa zilizoripotiwa tangu safari za Morogoro na Dodoma zianze ni za kutunga?
Kukwama kwa treni kisa ngedere na bundi ni uongo?
Kisingizio cha watu kuhujumu miundombinu ya reli pia ni uongo ulioshadidiwa na wajinga?

Sababu hasa ya kuendelea kuishi in denials ni nini? Badala ya kuyafanyia kazi mapungufu mnaamua kukaza shingo na kuita watu kuwa wajinga? Hiki kiburi chimbuko lake ni nini? 😲
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…