Elections 2010 Eti Vijana "CCM" wamwogesha mwenzao wa Chadema !

Elections 2010 Eti Vijana "CCM" wamwogesha mwenzao wa Chadema !

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Vijana "CCM" wamwogesha mwenzao Chadema - Habari Leo.

KUNDI la vijana tisa wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa CCM mjini hapa, wanadaiwa kumvamia kijana mkereketwa wa Chadema na kumvua nguo hadharani kisha kumpeleka mtoni kumwogesha kwa nguvu na kumnyoa nywele kwa kilichodaiwa ni ushabiki wa kisiasa.

Habari za uhakika kutoka eneo la tukio ambazo zilithibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage zilisema tukio hilo lilitokea Septemba 13 saa 6 mchana katika kijiji cha Tamasenga, Manispaa ya Sumbawanga ambapo kijana aliyekutwa na mkasa huo ni Festus Mizengo.

Inadaiwa kuwa kijana huyo ambaye ni muuza miwa katika kituo cha mabasi yaendayo Mbeya kijijini hapo wakati akiendelea na kazi yake huku akizungumza na mwenzake Robert Sikanda (3O), ghafla alivamiwa na kundi la vijana wapatao tisa na kuanza kumpiga kofi kisha kumvua nguo na kwenda kumwogesha mtoni.

Habari zinaeleza kuwa baada ya kuogeshwa, kijana huyo alinyolewa nywele kwa nguvu na kisha kupakwa mafuta ya samli, mwili mzima na kurejeshwa tena kijijini, huku vijana hao wanaoaminika ni wa CCM wakimwimbia wimbo wa ‘anameremeta’.

Baada ya kumaliza kitendo hicho vijana hao tisa walimwonya Mizengo kwa kumtaka aache kuishabikia Chadema vinginevyo watampa fundisho kali zaidi ya hilo.

“Bado haijajulikana chanzo cha tukio hilo, ingawa inasemekana kuwa ni ushabiki wa kisiasa, kwani inasemekana kuwa kundi hilo ni wafuasi wa CCM, wakati Mizengo na Sikanda ni wafuasi wa Chadema.

“Vijana hao inasemekana walikaririwa wakisema kushabikia Chadema ni uchafu ndio maana wakampeleka mwenzao mtoni kumwogesha,” alisema Kamanda Mantage.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, vijana hao wanahojiwa na Polisi juu ya tukio hilo, lakini alikataa kutaja majina yao kwa kile alichodai ni sababu za kiupelelezi na kwamba uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo unaendelea na wote waliohusika watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

My take: Jamani CCM inatupeleka wapi ! Angekuwa wa CCM ndio kafanyiwa hivi nina hakika hapangetosha kwani hii ingekuwa habari kubwa, lakini CCM mmh !
 
mm nnaona ni utani wa vijana tu


tuache kuyafanya makubwa, la wangemzuru hapo ingekuwa issue


hao ni vijana wenye kujuana
 
mm nnaona ni utani wa vijana tu


tuache kuyafanya makubwa, la wangemzuru hapo ingekuwa issue


hao ni vijana wenye kujuana
Ni utani? Ingekuwa vijana wa Chadema wamemfanzia hivyo mtu wa CCM na kumwonya aache kukumbatia chama cha mafisadi nina hakika usingesema ni utani.
 
Back
Top Bottom