Eti Watanzania ni wadokozi? Au Waajiri ndo wanyonyaji wanawalipa Watanzania kidogo?

Eti Watanzania ni wadokozi? Au Waajiri ndo wanyonyaji wanawalipa Watanzania kidogo?

..hao graduates wa Tanzania ni wezi wakiwa nchini kwao lakini wakiwa nje siyo wezi!!

..mbona kuna nchi kama Botswana na wakati fulani Zimbabwe Watanzania walikuwa wakiajiriwa kwa wingi tu?

..inawezekana Wakenya wakawa wako comfortable zaidi kuzungumza Kiingereza, lakini hiyo hailazimishi kuwaajiri wao na kuwaacha Watanzania.

..labda kinachowashinda Watanzania ni customer service lakini hilo ni suala ambalo mfanyakazi anaweza kujifunza kwa kuwa-exposed zaidi.
 
Pamoja na English kuwa moja ya sababu za kutokuajiriwa kwa waTanzania nchini mwao, sababu nyingine ni kama zifuatazo:

1. Mfanyakazi kujitolea zaidi katika kazi yake: Waajiri wengi huajiri watu wa nje ya nchi kwa kuwa mfanyakazi hutenga muda wake wote kwa kazi walizoajiriwa. Tofauti na mkazi wa eneo husika ambae hugawa muda wake katika kazi na familia

2. Ni rahisi kufuatilia mienendo ya mfanyakazi alietoka nje ya nchi kwa kuwa anakuwa muoga kuiba au kumkosea/kumfanyia maovu mwajiri wake kwa kuwa anakuwa hana connections katika maeneo ya kazi na hivyo, kuwa more reliable.

3. Mfanyakazi wa kutoka nje ya nchi ana nafasi ya kukaa muda mrefu na mwajiri wake. Hii ni kwa kuwa, anahitaji work Permit (ambayo mwajiri ndie anaemtafutia), na kurudi kwao ni gharama kubwa.

Hivyo, nakataa kuwa sababu ya kuajiriwa waKenya, Waganda na wengineo inatokana na kutokuwa wadokozi. Kwa waajiri wengi, udokozi si tatizo kubwa. Kwani wanajua jinsi ya kudhibiti hali hiyo au wanatakiwa kuwa na uwezo wa kuidhibiti.

Ni rahisi zaidi kumwajiri Mkenya katika mikoa ya Dar, Arusha, Kilimanjaro na kadhalika, kuliko kumwajiri Mganda, Mrwanda au Mrundi, kutokana na umbali wa nchi hizo nyingine. Ni rahisi kukuta katika mikoa ya Mwanza na Kagera waGanda, waRundi na/au Wanyarwanda wengi wakiajiriwa huko pia.

Tunachoweza kufanya ili kujihakikishia ajira ni kuwa reliable tu. Watu wengi huona fahari kuhamahama kazi kila mara. Hivyo waajiri huiona hiyo kuwa hatari kwa biashara zao.
 
Tunaongea hapa kama vile sio wasomi na critical thinkers, hapa kuna two way of thinking about kwanini Watanzania ni wadokozi, kwanza lazima tukubali kuwa watanzania ni wadokozi, statistically kima cha chini cha mtanzania nio sh. 100,000 lakini waajiri wengi wanalipa 60,000 mpaka 90,000 lakini matumizi ya mtu wa chini kabisa ni sh. 300,000 kwa mwezi. Hili linazibitisha ni jinsi gani watanzania walivyowezi, wanapata wapi difference ya kucover expenditute?

Then why wanaiba au ni wadokozi?

Mfumo mzima wa kazi tanzania haumsadii mfanyakazi kuwa mwaminifu kwa sababu zifuatazo:-

Moja, hakuna ulinganifu kati ya hali ya maisha na mshahara anaopewa mtanzania, unampa mtu 80,000 wakati unajua kabisa matumizi kwa mwezi ni 305,000 unataka wapi akatoe gap ya kiasi kilichobakia, psychologically mtu ataangalia mazingira yanayomzunguka na kujaribu kucover difference kutoka katika hayo mazingira, regardless ni legal au illegal. Solution ya hili ni kusynchronise statistics ilizonazo serikali then udokozi utapungua kwani naamini kuwa tatizo sio la taifa bali circumstances ndizo zinasababisha watu kuwa wadokozi.

Mbili, mfumo mzima wa mishahara umewafanya watu waamini kuwa mshahara kazini is not an issue, the issue is what extra income you get from job, nilikwenda kwenye interview somewhere interviewee baada ya kuongelea mshahara wakati tunasubiri kuitwa walikuwa wanaongelea extra income inayoweza kupatikana hapo, mentality ya watanzania siku hizi ni mapato ya ziada na sio mshahara, kusolve hili inatakiwa elimu ya kutosha ya uzalendo na uchumi kwa watanzania wote ili kuwarudisha kwenye msitari
 
Hivi hao Wakenya wametuzidi nini wabongo hadi wawe wanalipwa mishahara inayotuzidi? Mimi kila siku huku nakutana na Wakenya ambao sioni chochote walichonizidi. Sana sana ni wachovu na washamba na wanaotamani wangekuwa Watanzania. Sielewi kabisa hii ya kuwalipa mishahara iliyotuzidi

Lakini si umeomba kazi na kuikubali ukijua mshahara utakaopewa? Si kila kitu ni makaratasi. Uzoefu una uzito zaidi katika nyanja nyingi kuliko hayo makaratasi. Kama hautaki kupokea mshahara chini ya wakenya, acha kazi.

Mimi ningewashauri hao watanzania kuwa badala ya kung'ang'ania mishahara, wakazanie kwenye kujenga uzoefu utakaowawezesha kupambana na hao wakenya na wageni wengine. Na ndio, hako kasifa tunako. Wavivu, hatujitumi na wadokozi. Waulize Shoprite!

Amandla.......
 
Walipe watanzania au mtu yeyote vizuri hawezi kudokoa! Waajiri wanawalipa watanzania kiduchu sana ndiyo inapelekea kubuni mbinu ya udokozi ili Maisha yasonge mbele! Hao wageni wanaoajiriwa wanalipwa vizuri sana na wanakula raha ya maisha hawana sababu ya kudokoa
 
My bro, we have to face it. Hata mimi kama nikiwa na kampuni naweza kuajiri wakenya nitaacha watanzania. Hakuna kikubwa walichotuzidi wakenya, lakini kidogo walichotuzidi ni kikubwa sana kwa employers.

Kuna wabongo wavivu sana(wapo wachache wanafanya kazi vizuri sana), they are good at being puctual and attending to work, but they hardly work. Ajabu ni kuwa wanataka mishahara mikubwa. Udokozi ni moja ya sababu ambayo inatuponza sana wabongo, tuna mfano mzuri sana Shoprite, na kwenye mashirika mengi ya Tanzania, na hata serikalini. Tunajiibia hata wenyewe, so that makes it easy kuwaibia wageni.

Lakini tumejitakia sisi wenyewe, nani aliwapa vibali hao wakenya? ni sisi wenyewe? nani amewafanya hao employers wachague wakenya? ni sisi wenyewe.
Point ni kwa nini unaanza na mshahara mkubwa kwa mtu wa nje(mkenya)?na mtanzania kiduchu. kwa nini usifanye sawa kwa mtanzania ili tuone mwisho wa siku nani ana excel?experiment sahihi ni kwamba specimen zote ziwetreated equally(same mshahara, kazi, numba nk) ndo baadaye tu conclude kwamba utofauti umeletwa na utanzania. Watu mnajustify kuwanyonyo watanzania kwa dhana ya ni wavivu au wadogozi.Watanzania ni wadokozi. kitwete pia ni mtanzania kwaiyo ni mdokozi siyo?
 
Point ni kwa nini unaanza na mshahara mkubwa kwa mtu wa nje(mkenya)?na mtanzania kiduchu. kwa nini usifanye sawa kwa mtanzania ili tuone mwisho wa siku nani ana excel?experiment sahihi ni kwamba specimen zote ziwetreated equally(same mshahara, kazi, numba nk) ndo baadaye tu conclude kwamba utofauti umeletwa na utanzania. Watu mnajustify kuwanyonyo watanzania kwa dhana ya ni wavivu au wadogozi.Watanzania ni wadokozi. kitwete pia ni mtanzania kwaiyo ni mdokozi siyo?

Kwenye private sector hawa watanzania kawaita wadokozi,...sawa.., je wale watanzania wezi serikalini kama wa EPA,Kagoda, Rada, IPTL, TANESCO, Meremeta, Tenda za magari na Helicopter za jeshi tuwaiteje? Madokozi? Majongoo? au Matandu ya alhaji Mwinyi?... mkuu twaomba utupe jina sahihi kwa hao wahusika
icon6.gif
 
Hiyo ndiyo sera ya ajira ya CCM. Kapuya amewahi kutoa jibu hilohilo bungeni akieleza ni kwa nini wageni wanapewa ajira ambazo wa-Tanzania wana ujuzi wa kuzifanya!
 
Walipe watanzania au mtu yeyote vizuri hawezi kudokoa! Waajiri wanawalipa watanzania kiduchu sana ndiyo inapelekea kubuni mbinu ya udokozi ili Maisha yasonge mbele! Hao wageni wanaoajiriwa wanalipwa vizuri sana na wanakula raha ya maisha hawana sababu ya kudokoa

Tabia ya udokozi imejikita katika jamii yetu. Wazazi wetu walikuwa wakilipwa kiduchu lakini waliaminika. Leo hata hao wanaolipwa vizuri wanadokoa!

Amandla......
 
Na hii hoteli nasikia ni ya hao tunaowaita wazawa. Mnadhani wao ni wajinga kiasi hicho? Tunajuana na tunajua udhaifu wetu. Wakati umefika wa kukemea huu udhaifu ili turejeshe sifa waliyokuwa nayo wazazi wetu.

Amandla.....
 
Swali: Je watanzania ni wadokozi?

Jibu: Ndio kuna baadhi ya watanzania ni wadokozi na wengine wengi tu sio wadokozi. Na hii siyo tu kwa watu wa ngazi za chini, hata baadhi viongozi wetu wa ngazi za juu (yaani mawaziri, wabunge, makatibu wakuu, wakurugenzi etc.) ni wadokozi na kwa sasa hivi wamebatizwa jina la mafisadi. Kwa bahati mbaya habari mbaya huwa zinasambaa kwa haraka zaidi na hivyo habari kuhusu wafanyakazi wadokozi wa kitanzania zinasambaa kuliko zile za wafanyakazi waaminifu.

Swali: Je wageni wanaoajiriwa Tanzania ni wadokozi?

Jibu: Ndio kuna baadhi ya wageni ni wadokozi na wengine sio wadokozi. Ila inapotokea mgeni kadokoa mara nyingi huwa anarudishwa kwao na hivyo habari zao hazisikiki sana kama za wadokozi wenzao wa hapa nyumbani ambao hawana pa kukimbilia.

Swali: Je wakenya ni bora zaidi ya watanzania katika utendaji kazi za kila siku

Jibu:
  • Wakenya wengi wana ufahamu mzuri wa kiingereza kuliko watanzania wengi na hii inawapa nafasi nzuri zaidi ya kujiuza katika soko la ajira kuliko watanzania. Ndio kuna watanzania ambao ufahamu wao wa lugha ya kiingereza ni mzuri pengine kuliko wa wakenya wengi lakini hawa ni wachache sana kulinganisha na wenzetu.
  • Wakenya wako 'more agressive' katika kueleza thamani yao katika soko la ajira kuliko watanzania wengi ambao mara nyingi wanaona shida kujitathmini na kujua thamani yao katika soko la ajira. Nimebahatika kushiriki kwenye 'interviews' ambapo mtu anaulizwa angependa kulipwa kiasi gani anajibu kuwa yuko tayari kupokea chochote ambacho mwajiri atampatia. Kwa mfumo nyonyaji wa sasa lazima mwajiri atakupunja tu.
  • Wafanyakazi wakenya hasa kwenye sekta ya mahoteli wanajituma zaidi ya wenzao watanzania katika kufanya kazi. Hii ni rahisi kuona unapofika hotelini ambapo hapa nyumbani inabidi mpaka uombe msaada wa kubebewa mzigo wakati kwa wenzetu akikuona tu anachangamkia mzigo bila ya kuombwa. Nadhani attitude yetu katika kazi inahitaji maboresho ya hali ya juu ili kuweza kushindana na wenzetu wageni wanaokuja kufanya kazi hapa nchini.
Swali: Je ni sawa kwa Rais kuongelea suala la udokozi wa watanzania?

Jibu: Ndio na hapana. Kwanza hii siyo mara ya kwanza kwa rais wa Tanzania kuongelea suala hili. Nakumbuka raisi Mkapa alikwishawahi kulizungumzia hili na alitumia jina la 'mabazazi' kuelezea wadokozi wa kitanzania. Nadhani suala la msingi ni kuwa raisi anaongelea hili kwa malengo gani. Jambo la kujiuliza ni kwamba: je anaongelea suala hili ili kuhalalisha uajiri wa wageni nchini au anaongelea hili kuwataka watanzania wajifanyie tathmini ili kupata suluhu ya tatizo za udokozi katika jamii yetu kuanzia ngazi ya chini mpaka viongozi wa ngazi za juu?. Nashawishika kuamini kuwa rais aliongelea suala hili kuhalalisha ajiri za wageni nchini kutokana na hadhira aliyokuwa nayo wakati akiongea maneno hayo. Mimi siamini kuwa suluhu ya udokozi ni kuajiri wageni. Na kama suluhu ya udokozi Tanzania ni kuajiri wageni basi ni vyema tukapanua wigo wa ajira ya wageni katika ngazi zote zikiwemo za kisiasa kama uwaziri, ukatibu mkuu, ukuu wa mikoa, ukurugenzi wa wizara na hata urais.
 
Aaah wapi! mimi nakataa katakata. Wakenya hawajatuzidi lolote. Basi tu sisi tuna matatizo yetu ya kutukuza vya nje. Ujinga mtupu.
Viongozi wetu nao huwapendelea wageni kuliko watanzania kwa sababu wanatafuta wabia wa kuwasaidia kutuibia rasilimali zetu. Hali hii inathibitishwa na ukweli kwamba sifa ya kuwa muwekezaji hasa kwenye makampuni yaliyokuwa ya umma ni kuwa mgeni. Sababu ziko wazi mtanzania pesa za kuhonga utazipata wapi? Na wakati huohuo habari za ufisadi huo ukimfanyia mtanzania zitavuja tofauti na mgeni.
 
Juzi Snow Crest Imefunguliwa Arusha, na wafanyakazi wageni wameajiriwa kwa wingi. Na Watanzania wameitwa wadokozi

Sababu ni nini??

Watanzania ni Wadokozi? Au Waajiri ndo wanyonyaji wanawalipa watanzania mshahara kidogo ukilinganisha na wageni.

Mfano Mshahara wa Graduate wa Kitanzania ni laki 3 while graduate wa Kenya Au Ulaya ni Millioni moja??

Huyo Mtanzania ataweza kupanga nyumba ya hadhi yake? Ataweza kupanda gari ya hadhi yake? Mtanzania ataweza kujiwekea akiba ili baadae ajenge nyumba au anunue gari au asomeshe watoto?

Kwa hiyo Wadau hapa JF jadilini kama Watanzania ni wadokozi kweli au Watanzania wanaonewa??

...kulipwa kidogo kusiwe sababu ya waajiriwa kuwa wadokozi bana, huko ni kutetea ujinga. mfano, Pale Lamada Apartments kila leo wageni wanaibiwa,... menejimenti inadai eti 'Valuables should be kept at Hotel's reception',...maana yake ukiibiwa nguo, viatu nk kule vyumbani it's at your own risk au?
 
Zakumi, kwani Kiingereza kwa Wakenya sio lugha ya pili au ya tatu? Kama ni hivyo basi hakuna tofauti sana na Watanzania. Hivi umewahi kumsikia raisi wao akiongea Kiingereza? Hata Kikwete ana afadhali!

Still, mimi bado sijashawishika kuwa eti Wakenya wanatuzidi. Mimi kila siku nawaona na sioni lolote spesheli walichonacho. Wanazimia Kiswahili changu na Kiingereza changu cha kubabaisha. Haki ya nani tena Wakenya hawatuzidi kabisa! Tatizo tulilonalo (Watanzania kwa ujumla) labda ni perceptions tu. Perceptions tulizonazo ni kwamba wanatuzidi (supposedly wanaongea kiingereza kizuri-kitu ambacho nakataa) wakati actual reality ni kwamba hawatuzidi lolote.

Juli:

Kazi nyingi tunazolalamikia humu ndani zipo kwenye service sectors. Hizi kazi kwa kweli watanzania hatuna traditions nazo.

Michipuo mingi ya elimu Tanzania inawaandaa watu kuwa mabwana shamba, mainjinia, madaktari, watabibu, bwana misitu. Hivyo lugha zetu zipo rounded kwenye masuala hayo.

Lakini kwenye masuala ya service we are not so good.
 
Aaah wapi! mimi nakataa katakata. Wakenya hawajatuzidi lolote. Basi tu sisi tuna matatizo yetu ya kutukuza vya nje. Ujinga mtupu.

...lugha tu baba, lugha ya kuji express mbele ya wageni ndio kimbembe.
 
Juli:

Kazi nyingi tunazolalamikia humu ndani zipo kwenye service sectors. Hizi kazi kwa kweli watanzania hatuna traditions nazo.

Michipuo mingi ya elimu Tanzania inawaandaa watu kuwa mabwana shamba, mainjinia, madaktari, watabibu, bwana misitu. Hivyo lugha zetu zipo rounded kwenye masuala hayo.

Lakini kwenye masuala ya service we are not so good.

Kwenye hilo sina ubishi maana concept ya customer service bongo bado ni foreign.
 
Lakini si umeomba kazi na kuikubali ukijua mshahara utakaopewa? Si kila kitu ni makaratasi. Uzoefu una uzito zaidi katika nyanja nyingi kuliko hayo makaratasi. Kama hautaki kupokea mshahara chini ya wakenya, acha kazi.

Mimi ningewashauri hao watanzania kuwa badala ya kung'ang'ania mishahara, wakazanie kwenye kujenga uzoefu utakaowawezesha kupambana na hao wakenya na wageni wengine. Na ndio, hako kasifa tunako. Wavivu, hatujitumi na wadokozi. Waulize Shoprite!

Amandla.......

Kamanda FM:

Matatizo mengi yapo jinsi tunavyojiandaa. Tunapenda short cuts. Watanzania wengi wanatafuta kazi hili baada ya mwaka awe amejenga nyumba nzuri, amenunua gari mbili, firiji, amepata mke na watoto kwa kutumia CASH. Matokeo ni wizi na rushwa za kipuuzi.
 
Swali: Je watanzania ni wadokozi?
Jibu: Ni katika mazingira yapi na gani iwafanye wadokozi?

Swali: Je wageni wanaoajiriwa Tanzania ni wadokozi?

Jibu:Jiulize kwanza nawe ujijibu mkuu iweje mhindi afanye kazi ya kuwa chef na akaweza kujenga nyumba kwao india ndani ya mwaka mmoja ktk hotel??Huo mshahara wake itakuwa ni mara ngapi na mtanzania?? na mazingira ya kazi yake yakoje na ukilinganisha na ya mtanzania??

Swali: Je ni sawa kwa Rais kuongelea suala la udokozi wa watanzania?

Jibu:Ana haki ya kuongea ila alipaswa kuwa na Details za kutosha na aongeee hilo, ila me ni kuwa amejishusha ki uongozi, au naye anamaslahi katika kitegauchumi hicho.


Swali:Je IKULU ilikuwa haina taarifa kuwa Snow Crest Hotel eneo la parking lilikuwa limeingia eneo la barabara.

Swali:Je Protocal Utendaji wao wakazi ni Sanifu au?

Swali: Je uhamiaji wanatoa vibari halali kwa waafanyakazi wa kigeni? na muda wao wa kufanya kazi ndani ya nchi yetu ni muda gani?

Swali: Mfano katika hotel mmoja tu experts wanatakiwa kuwa wangapi?

Swali: Katiba yatu yan nchi ianaeleza vipi kumwajiri expert?

Swali: Ilani ya CCM inasena vipi kuhusu ajira kwa watanzania?




 
Jibu:Jiulize kwanza nawe ujijibu mkuu iweje mhindi afanye kazi ya kuwa chef na akaweza kujenga nyumba kwao india ndani ya mwaka mmoja ktk hotel??Huo mshahara wake itakuwa ni mara ngapi na mtanzania?? na mazingira ya kazi yake yakoje na ukilinganisha na ya mtanzania??

Jethro, hauwezi kulinganisha gharama za kujenga India na bongo. Wale bado wanajengea matofali ya kuchoma, vigae vya udongo ni bei ya chini na labour cost ndiyo usiseme! Sisi tunauziana nyumba ya vyumba viwili kwa dola laki mbili! Go figure!

Amandla.....
 
Rais ameongea non sense, inabidi ataombe radhi agh!

Yaani kwa sample yake ya kuuliza mwenye wote moja tu ameamua ku-generalize kwamba wa Tanzania wote ni wadokozi ujinga huu ala..wengine tunakula vya halali from day one na wako wengi tu !
 
Back
Top Bottom