Hivi hao Wakenya wametuzidi nini wabongo hadi wawe wanalipwa mishahara inayotuzidi? Mimi kila siku huku nakutana na Wakenya ambao sioni chochote walichonizidi. Sana sana ni wachovu na washamba na wanaotamani wangekuwa Watanzania. Sielewi kabisa hii ya kuwalipa mishahara iliyotuzidi
Point ni kwa nini unaanza na mshahara mkubwa kwa mtu wa nje(mkenya)?na mtanzania kiduchu. kwa nini usifanye sawa kwa mtanzania ili tuone mwisho wa siku nani ana excel?experiment sahihi ni kwamba specimen zote ziwetreated equally(same mshahara, kazi, numba nk) ndo baadaye tu conclude kwamba utofauti umeletwa na utanzania. Watu mnajustify kuwanyonyo watanzania kwa dhana ya ni wavivu au wadogozi.Watanzania ni wadokozi. kitwete pia ni mtanzania kwaiyo ni mdokozi siyo?My bro, we have to face it. Hata mimi kama nikiwa na kampuni naweza kuajiri wakenya nitaacha watanzania. Hakuna kikubwa walichotuzidi wakenya, lakini kidogo walichotuzidi ni kikubwa sana kwa employers.
Kuna wabongo wavivu sana(wapo wachache wanafanya kazi vizuri sana), they are good at being puctual and attending to work, but they hardly work. Ajabu ni kuwa wanataka mishahara mikubwa. Udokozi ni moja ya sababu ambayo inatuponza sana wabongo, tuna mfano mzuri sana Shoprite, na kwenye mashirika mengi ya Tanzania, na hata serikalini. Tunajiibia hata wenyewe, so that makes it easy kuwaibia wageni.
Lakini tumejitakia sisi wenyewe, nani aliwapa vibali hao wakenya? ni sisi wenyewe? nani amewafanya hao employers wachague wakenya? ni sisi wenyewe.
Point ni kwa nini unaanza na mshahara mkubwa kwa mtu wa nje(mkenya)?na mtanzania kiduchu. kwa nini usifanye sawa kwa mtanzania ili tuone mwisho wa siku nani ana excel?experiment sahihi ni kwamba specimen zote ziwetreated equally(same mshahara, kazi, numba nk) ndo baadaye tu conclude kwamba utofauti umeletwa na utanzania. Watu mnajustify kuwanyonyo watanzania kwa dhana ya ni wavivu au wadogozi.Watanzania ni wadokozi. kitwete pia ni mtanzania kwaiyo ni mdokozi siyo?
Walipe watanzania au mtu yeyote vizuri hawezi kudokoa! Waajiri wanawalipa watanzania kiduchu sana ndiyo inapelekea kubuni mbinu ya udokozi ili Maisha yasonge mbele! Hao wageni wanaoajiriwa wanalipwa vizuri sana na wanakula raha ya maisha hawana sababu ya kudokoa
Viongozi wetu nao huwapendelea wageni kuliko watanzania kwa sababu wanatafuta wabia wa kuwasaidia kutuibia rasilimali zetu. Hali hii inathibitishwa na ukweli kwamba sifa ya kuwa muwekezaji hasa kwenye makampuni yaliyokuwa ya umma ni kuwa mgeni. Sababu ziko wazi mtanzania pesa za kuhonga utazipata wapi? Na wakati huohuo habari za ufisadi huo ukimfanyia mtanzania zitavuja tofauti na mgeni.Aaah wapi! mimi nakataa katakata. Wakenya hawajatuzidi lolote. Basi tu sisi tuna matatizo yetu ya kutukuza vya nje. Ujinga mtupu.
Juzi Snow Crest Imefunguliwa Arusha, na wafanyakazi wageni wameajiriwa kwa wingi. Na Watanzania wameitwa wadokozi
Sababu ni nini??
Watanzania ni Wadokozi? Au Waajiri ndo wanyonyaji wanawalipa watanzania mshahara kidogo ukilinganisha na wageni.
Mfano Mshahara wa Graduate wa Kitanzania ni laki 3 while graduate wa Kenya Au Ulaya ni Millioni moja??
Huyo Mtanzania ataweza kupanga nyumba ya hadhi yake? Ataweza kupanda gari ya hadhi yake? Mtanzania ataweza kujiwekea akiba ili baadae ajenge nyumba au anunue gari au asomeshe watoto?
Kwa hiyo Wadau hapa JF jadilini kama Watanzania ni wadokozi kweli au Watanzania wanaonewa??
Zakumi, kwani Kiingereza kwa Wakenya sio lugha ya pili au ya tatu? Kama ni hivyo basi hakuna tofauti sana na Watanzania. Hivi umewahi kumsikia raisi wao akiongea Kiingereza? Hata Kikwete ana afadhali!
Still, mimi bado sijashawishika kuwa eti Wakenya wanatuzidi. Mimi kila siku nawaona na sioni lolote spesheli walichonacho. Wanazimia Kiswahili changu na Kiingereza changu cha kubabaisha. Haki ya nani tena Wakenya hawatuzidi kabisa! Tatizo tulilonalo (Watanzania kwa ujumla) labda ni perceptions tu. Perceptions tulizonazo ni kwamba wanatuzidi (supposedly wanaongea kiingereza kizuri-kitu ambacho nakataa) wakati actual reality ni kwamba hawatuzidi lolote.
Aaah wapi! mimi nakataa katakata. Wakenya hawajatuzidi lolote. Basi tu sisi tuna matatizo yetu ya kutukuza vya nje. Ujinga mtupu.
Juli:
Kazi nyingi tunazolalamikia humu ndani zipo kwenye service sectors. Hizi kazi kwa kweli watanzania hatuna traditions nazo.
Michipuo mingi ya elimu Tanzania inawaandaa watu kuwa mabwana shamba, mainjinia, madaktari, watabibu, bwana misitu. Hivyo lugha zetu zipo rounded kwenye masuala hayo.
Lakini kwenye masuala ya service we are not so good.
Lakini si umeomba kazi na kuikubali ukijua mshahara utakaopewa? Si kila kitu ni makaratasi. Uzoefu una uzito zaidi katika nyanja nyingi kuliko hayo makaratasi. Kama hautaki kupokea mshahara chini ya wakenya, acha kazi.
Mimi ningewashauri hao watanzania kuwa badala ya kung'ang'ania mishahara, wakazanie kwenye kujenga uzoefu utakaowawezesha kupambana na hao wakenya na wageni wengine. Na ndio, hako kasifa tunako. Wavivu, hatujitumi na wadokozi. Waulize Shoprite!
Amandla.......
Jibu: Ni katika mazingira yapi na gani iwafanye wadokozi?Swali: Je watanzania ni wadokozi?
Swali: Je wageni wanaoajiriwa Tanzania ni wadokozi?
Swali: Je ni sawa kwa Rais kuongelea suala la udokozi wa watanzania?
Jibu:Jiulize kwanza nawe ujijibu mkuu iweje mhindi afanye kazi ya kuwa chef na akaweza kujenga nyumba kwao india ndani ya mwaka mmoja ktk hotel??Huo mshahara wake itakuwa ni mara ngapi na mtanzania?? na mazingira ya kazi yake yakoje na ukilinganisha na ya mtanzania??