PreGE2025 Eugen Kabendera: Wamekuja CHAUMMA wapate Ubunge wa kupewa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kabendera anawalaumu waliojiunga na Chaumma kwa kusema wazi kuwa nia yao ni kugombea ubunge. Hawajaanza leo kufanya hivyo. Na walipopata nafasi ya kupata ubunge waliwapigania sana watanzania na walisimamia vizuri serikali.

Kupata ubunge ni process. Hawa itabidi wafanye kampeni kuwaelezea wananchi kwa nini wanaamini kuwa CCM haifai na watawafanyia nini wananchi wakiwachagua. Kugombea wao ubunge hakumaanishi kuwa ni lazima wataupata.

Tofauti yao na CDM nk kuwa wanaonyesha kuwa wako tayari kupambana hata katika mazingira ambayo wanajua taika kuwa yatakuwa magumu.

Chadema haitakuwa na nafasi hiyo maana watajulikana kuwa hawana namna ya kuyafanikisha maana watakuwa nje ya Bunge. Wote tumeona jinsi Aidan alivyo pambana katika mazingira magumu. Wakipatikana hata Aidan wawili iyakuwa afadhali kuliko kushinda kwenye makongamano Ulaya.

Amandla...
 
ni kweli wale hawawezi kupata kura halali, chauma haina rekodi za kupata wabunge, labda wapewe ubunge wa bwerere ki manuever
 
Hayo wameenda kukichukua chama cha chauma,wanasubiri bosi wao mbowe aje kisha wamalizane na mzee wa ubwawa.
mbowe asitake kufanya siasa za mazingaombwe namna hiyo, ni bora akaendelea kukaa kimya tu au aachane na siasa kuliko kwenda kujititimua chauma kufanya siasa za kilaghai
 
Ni suala la muda tutashuhudia siasa za kitapeli
 
Ubunge kwa sasa umepoteza hata maana yake, kwamba Mbunge atachaguliwa na Wananchi, lakini imekuwa Ubunge ni hisani ya raisi na mapolisi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…