EVE - (Ruff Ryders First-lady )

I_manyota

Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
48
Reaction score
44
Eve Jihan Jeffers Cooper au wengin tunamjua kama EVE, rapper wa kike kutoka nchini Marekani, Philadelphia huko kwa kina Meek Mill na wengine wengi. Watoto wa 2000's ni ngumu kumjua huyu mwanamama unless uwe unapenda kusikiliza ngoma ambazo zilikua zina heat kipindi unazaliwa πŸ˜‚ πŸ˜‚, usinune bhana ila ndio ukweli huo nyie mnawajua kina Cardi B na Minaj ukiulizwa kuhusu hawa unaweza ukabaki unatoa macho tu hapo sasa kamata hapa.

Kwa haraka haraka Eve miaka hyo ya 2000's alisumbua sana kwenye game la Hip-hop si kinadada wenzie au masela ukimshirikisha Eve uwe umejipanga maana bi alikua anajua kuandika na kupasuka vile vile ukitaka 101 battle huko ndio hata usiguse kabisa anakuvua nguo kama hukujipanga.


Eve alizaliwa mwaka 1978, huku mama yake akiwa bado binti tu wa miaka 17, Eve anasema alianza muziki akiwa na miaka 11-12 hivi yeye na rafiki yake wakaunda Dope Girls ambapo waliendelea mpaka walipkuwa high school (Martin Luther King High School ). Eve alipenda sana kurap hasa battle rap, yaani yeye ukimwambia mambo ya kubato ulikua unamkosha na alikua anajua haswaa.
I was a battle rapper, i wanted to go up against all the guys in every cypher on every corner, like I've always been a tomboy.
I did what i had to do i proved to y'all, females to do with milk to do only better
Life la shule likaisha ilimbidi Eve kuingia mtaani kusaka mkwanja, akiwa na miaka 18 eve alianza kazi kama stripper japo aliifanya kwa kipindi kifupi kama mwezi hivi, unajua tena haikua kitu ambacho alipenda kufanya hata wakati anafanya anasema yeye ndio alikua stripper goigoi kiasi wateja kutomkubali sana. Ila Eve hajawahi kujutia kitendo hicho maana anasema alikua kwenye harakati za kutafuta so haimuumizi kichwa.

Lakini ya Mungu ni mengi unajua kama ndio hapo ambapo palimfanya Eve aanze kuona mwanga katika kipaji chake unaambiwa night moja mzee baba Mase akatimba hiyo Club ambayo Eve alikua akipiga mzigo. Aaah madogo nimesahau kumbe na huyu mjuba hamumjui. Mase alikua rapper wa Badboys Ent. hii ya P. Diddy miaka hiyo alisumbua sana na yeye kwenye game la hipo-hop.
.

Haya bhana mzee baba kingia si akaona mtoto mkali, unajua tena ikabidi mjuba aanze kuchombeza chombeza, Eve anakwambia alikua hamuelewi jamaa sababu hata alikua hamjui mchizi full kumpa majina ya uwongo na namba za uwongo.

Meneja wake Eve alikua na rafiki yake ambaye alikua akifanya kazi na Dre. Dre ,ukafanyika mpango Eve akutane na jamaa amsikie mwenyewe so ilikua kama audition flani hivi. Basi bhana beat ikawekwa mtoto wa kike akaanza kuspit jamaa hakutaka kusubiri akaukubali uwezo wake
She give me one verse and hoot, and told her i said that's it i don't need to hear anymore, basically have two weeks get your bags packed you're coming back to L.A
Kipindi Eve anasainiwa AfterMath Rec rapper Eminem nae akawa amesaini kipindi hicho hicho Dre alimkubali sana Eminem kiasi muda mwingi aliutumia kufanya kazi na Eminem na kumsahau Eve. So kwa lugha fupi Eminem alitia kitumbua mchanga
There's nobody out there that's that's even close to what he's doing
Baada ya kukaa kwa muda hivi Dre aliamua kusitisha mkataba na Eve, ila Jimmy Iovine Co-founder Chairman Interscope Records alimkubali Eve na hakutaka kuona dogo anabaki kitaa wakati ana kijpaji kikubwa sana basi jamaa na Dre wakaona bora wamfanyie mpango na Ruff Ryders Records, basi waka link na ruff ryder wakapigiwa simu aende Yonkers, New York.

Unaambiwa baada ya kufika wakaenda zilipo studio humu ndani walikua wamekaa masela tupu kina DMX, JADA wasanii wote waliokuwa chini ya label ya Ruff Ryders, na sababu ilikua ni kumfanyia interview ambayo ilikua ni lazima ubato na wale jamaa ukiweza kuwamudu basi wewe umepita.

We go to powers house and i'm walking up in the studio with all these guys, there was, Raw there was D i mean everybody was there
Everybody had a battle to become Ruff Ryders. you're going to be very uncomfortable or you're going to be comfortable.
Shughuli ikawa imeishia hapo mdada akatisha sana mule ndani wana wakamkubali akala mkataba wake akawa msanii wa kwanza wa kike kusainiwa na Ruff Ryders.

I was the first lady of Ruff Ryders so it was important for me that they saw that i am going to hustle the way you guys hustled period. Do not separate me and they didn't.

Mwaka 1999 Eve akawa amerokodi album yake ya kwanza LET THERE BE EVE album ambayo aliindika eve mwenye na iliyobeba historia ya maisha yake.

 
Ile tattoo yake kwenye nyonyo ilikua inanikosha sana
 
Who's that girl...EVE anajua sana...kuna ngoma ya Luda inaitwa My Chick Bad Rmx hiyo mdada EVE yupo umo amefunika mbaya wadada wenzie maana humo kuna wadada tupu Luda yupo kwenye Chorus tu.
 
Who's that girl...EVE anajua sana...kuna ngoma ya Luda inaitwa My Chick Bad Rmx hiyo mdada EVE yupo umo amefunika mbaya wadada wenzie maana humo kuna wadada tupu Luda yupo kwenye Chorus tu.
 
Love is Blind katika ngoma zake zote naikubali hii kuliko zote. Mpaka leo ipo kwenye playlist langu
 
Pamoja kuwa na mashairi mazuri, alikuwa ananikosha zaidi na ile flow yake.. Jinsi anavyonata na beat aisee, huyu mlimbwende alikuwa ananikosha..

Vile vinyonyo vyake na ile tattoo, udenda ulinitoka saana.

My chick is bad aliwafunika mbaya kina nick na wenzie.
 
game ilikuwa ipo sawa kipind kile kule kuna mc lite. huku kuna left eyes hapa kuna miss eliot yan una enjoy music sio takataka hizi za saiz
 
Ile beat ya gotta man wacha kabisa
 
I think alirudi kwa dre kutengeneza Let me Blow your mind

Nimeskiliza sana Let there be Eve, dem ana mistari sana Ila Swiss Beats hakuwa mbunifu sana kumtengenezea beats nzuri

Album ilikua nzuri tatizo ilikuja wakati mmoja na I am ya Nas, Slim Shady LP ya Eminem na Vol 3: Life and times of S. Carter ya Jay Z

Hiyo miamba iliachia album kali sana kwa wakati huo, competition ilikua kali kwenye mauzo

1999 - 2000 ilikua season ya ngoma kali tu
 
Nishamshuhudia 2008/09 show yake,alikuja na Fat Joe.
 
Eve ft Alicia keys

Gangster loving ...acha kabisa hii ngoma
 
Huyu dada nilikuwa namkubali saaana yani. Kuna wakati nilisikia alikuwa dem wa mtoto wa rais wa Equatorial Guinnea. Sijui waliishiaga wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…