Everton vs Saigon 1967

Mo Said,wewe ni kisima cha historia, document hiyo elimu yako ili vizazi vya sasa na vijavyo vinufaike
Mixo...
Ingia hapo chini uangalie kila kitu kimehifadhiwa bila hati miliki tumia upendavyo hiyo ni sadaka kwa niaba ya wapigania uhuru wote wa Tanzania:


mohamedsaidsalum.blogspot.com
mohamedsaidsalum.com
 
Heshima nyingi sana kwako mkuu.
 

Sihitaji hata kuwajua hata ungeandika gazeti refu kiasi gani.

Kama mlimpokea mjini na akawazidi akili ndio mjiulize uwezo wenu wa akili ukoje.

Asante sana Mwl Nyerere.
 
Sihitaji hata kuwajua hata ungeandika gazeti refu kiasi gani.

Kama mlimpokea mjini na akawazidi akili ndio mjiulize uwezo wenu wa akili ukoje.

Asante sana Mwl Nyerere.
Wa...
Sidhani kama hili ni tatizo la mtu mmoja kumzidi akili mwingine.

Ndipo niliposema hutujui.

Nifahamishe Nyerere katuzidi sisi akili katika nini?

Wazee wetu wangekuwa hawana akili wasingeweza kuunda African Association (AA) 1929, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika)1933 na TANU 1954.

Kleist Sykes rafiki ya babu yangu kaacha historia nzima ya mapambano ya Waafrika wa Tanganyika dhidi ya ukoloni aliyoandika kabla hajafa 1949 kama mswada wa kitabu, "Kleist Sykes The Townsman," (1968).

Hii ni seminar paper inapatikana Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana mwandishi Aisha "Daisy" Sykes, mjukuu wake bint ya Abdulwahid Kleist Sykes.

Hivi sasa ni sura katika kitabu alichohariri John Iliffe, "Modern Tanzanians, " (1973).

Mimi nikamwandika upya Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography (DAB) Oxford University Press, New York 2011.

Babu yangu Salum Abdallah alikuwapo ndani ya AA Dar es Salaam kuanzia 1929 hadi 1947 alipohamia Tabora.

Kuanzia 1947 - 1960 aliongoza migomo mikuu mitatu ya wafanyakazi wa reli wa mwisho 1960 ulidumu siku 82.

Alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU Western Province, Rais muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU)1955 na aliunganisha TRAU na TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana 1961.

Labda nikuongezee kitu babu yangu Salum bin Abdallah alikuwa mfadhili mkubwa wa harakati zote hizi.

Kama unauliza uwezo wa akili zetu ushahidi ni huo hapo juu na babu yangu alikuwa mkulima na mfanyabiashara juu ya kuwa politician na trade unionist.

Babu yako ana historia gani?
Hana kitu.

Unaweza ukasimama mbele ya watu ukajinasibu na babu yako?

Huwezi na sababu ni kuwa huna cha kueleza katika maisha yake.

Je, ungependa nimwite babu yako mjinga, mshamba, mbumbumbu Mzungu wa Reli?

Hiyo picha hapo chini kulia ni Kassanga Tumbo Katibu Muasisi wa TRAU anaefuatia ni babu yangu Salum bin Abdallah Popo Rais Muasisi wa TRAU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

 

Babu yangu hakuwahi kukaribisha mtu mjini afu akamzidi akili.Endeleeni kula maandazi na kukaa kibarazani huku mkijiita ni watoto wa mjini.

Nyerere aliwazidi akili kwny kila kitu,na ndio maana ni baba wa taifa hili.Nyie nani anawajua nchi hii?labda huko kwny vijiwe vya kahawa kariakoo ndio mnajulikana.
 
 
Wa...
Babu yako wewe ndiye unaemfahamu.

Mimi nimekuuliza je babu yako anayo historia katika kupigania uhuru wa Tanganyika?

Sisi tuna historia ya kuikomboa Tanganyika kutoka makucha ya ukoloni.

Ukitutafuta Google utatukuta halikadhalika, Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Library of Congress, Washington DC.

Kukaribisha mtu mjini hili linafanyika kila siku.

Babu yako alimkaribisha nani?
Huna.

Naona unaandika umechukia unatoa matusi ilhali mimi nakueleza historia ya wazee wangu ambayo ni historia ya uhuru wa Tanganyika.

Hili si jambo la kukuchukiza labda ikiwa moyo wako umejaa hasad.

Hili la kukaa barzani na kunywa kahawa iko katika mila zetu sawa na labda kwenu kwenda kilabu cha pombe kulewa nyakati za jioni.

Mimi sina haki ya kuwazomea kwa kunywa kangara kwani huo ni utamaduni wenu kama kahawa ilivyokuwa utamaduni wetu.

Hili la uenyeji wa Dar es Salaam na utoto wa mjini mimi sijivunii hilo kwani sikuchagua wapi nizaliwe ni Allah ndiye aliyepanga hivyo.

Nitachekesha watu ikiwa mimi nitajinasibu kwa kuzaliwa mjini watu wakisikia watanitoa hamnazo.

Hili la kujulikana wala sitalisemea chochote kwani halima maana yeyote.

Hiyo picha hapo chini ni mimi niko Library of Congress, Washington DC.

 
Maashallaa jibu la hekima kabisa
Tan...
Huyu ndugu yetu yeye alidhani akisema kuwa Saigon ni chama cha Waislam mimi nitapata hofu na kukana.

Hapo ndipo nilipojua kuwa ndugu yangu ni mgeni na kuna mengi asiyojua.

Saigon tumeiunda 1967 tena wastani wa umri wetu miaka 15/16 wengi wetu tuko shule ya msingi.

Club yetu ilikuwa Mtaa wa Narung'ombe, Kariakoo.

Wakazi wote wa Kariakoo, Gerezani na kwingi Dar es Salaam, Buguruni, Temeke wakati ule walikuwa Waislam.

Hili yeye kaliona kioja ndiyo anashangaa iweje Saigon iwe Waislam watupu?

Hakuwa anajua kuwa Wengine walikuwapo lakini makazi yao ilikuwa Misheni Kota.

Sikumlaumu nilijua tutaelimishana lakini bahati mbaya inaelekea ndugu yetu kajaa chuki.

Msome maneno yake.
 
Maalim tujuze kuhusu aliyempigia chapuo Mkapa ktk raund ya pili baada ya kushindwa ya kwanza
 

Hahahahah maneno meeeengi unaenda kupiga picha kwny congress ya makafiri?

Narudia tena babu yangu hakua mla kashata na kahawa barazani kuanzia asubuhi to jioni,hayo ni ya wakina dosa na nyie.
 
Hahahahah maneno meeeengi unaenda kupiga picha kwny congress ya makafiri?

Narudia tena babu yangu hakua mla kashata na kahawa barazani kuanzia asubuhi to jioni,hayo ni ya wakina dosa na nyie.
Wa...
Ndugu yangu nachokiona kwako ni tatizo la uungwana na labda niongeze kuwa hunifahamu mimi wala wazee wangu.

Babu yako unasema hakuwa mla kashata.
Sawa.

Unasema hakuwa mkaa barazani kuanzia alfajir hadi maghrib.

Sawa.

Lakini nimekueleza babu yangu alikuwa nani.

Babu yangu Salum Abdallah alikuwa mwanachama wa AA, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, TAA na pia muasisi wa TANU.

Babu yangu alikuwa muasisi wa TRAU kiongozi wa watu na mfadhili wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nyumbani kwake kulikuwa na barza kubwa sana ya wana TANU na kahawa na kashata ikinyweka sana hapo.

Nimekufahamisha pia kuwa babu yangu juu ya kuwa mpigania uhuru alikuwa mfanyabiashara na mkulima.

Kipi kinachokushinda wewe kumweleza babu yako?

Umemtaja Dossa Aziz.

Babu yangu alikuwa na nyumba yake Mtaa wa Congo na Mbaruku katika miaja ya 1930 jirani na nyumba ya Aziz Ali baba yake Dossa.

Dossa na baba yangu wamecheza pamoja udogoni.

Unapomkejeli Dossa umemkejeli baba yangu.

Hapa kwenye huu mjadala baina yangu na wewe haya maneno ya "makafiri," ya kutukana imani na dini za watu yanaingia vipi?

Mimi sikuenda Library of Congress "kupiga picha," nilikuwa hapo na Capitol Hill katika utafiti na katika miaka yangu ya uanafunzi nilikuwa member wa maktaba hiyo.

Ndugu yangu si ungefanya hata juhudi kidogo unijue ujiondolee fedheha ya kuropoka?

Hii picha hapo chini niko Northwestern University, Evanston Chicago, Illinois nilialikwa kufanya mhadhara.




Capitol Hill Washington DC
 
Hahahahah maneno meeeengi unaenda kupiga picha kwny congress ya makafiri?

Narudia tena babu yangu hakua mla kashata na kahawa barazani kuanzia asubuhi to jioni,hayo ni ya wakina dosa na nyie.
We jamaa sasa unazingua ,kama hupendi kilchoandikwa ebu sepa na wewe ukaandike yako.watu hapa tunatakuja kujua ivi vitu.

Sent from my SM-G960F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna haja ya kumjibu huyu jamaa,inawezekana unajibishana na kinda alozaliwa 90's.

Sent from my SM-G960F using JamiiForums mobile app
 
Subiri jina la ustaadhi hapo linaletwa.
Wa...
Mimi elimu ya mwanzo aliyonifunza mama yangu ni adabu yaani kuheshimu watu.

Nilipokuwa sasa nasoma nilifunzwa ilm ya mjadala katika madras na somo hili lina kipengele cha "Adabu ya Elimu."

Mwalimu wangu alikuwa Sheikh Haruna.
Alikuwa akinambia, "Mohamed ukitukana watu umenitukana mimi mwalimu wako na umemtukana mama yako."

Siku moja nikamuuliza, "Sheikh naelewa kukutukanisha wewe mwalimu wangu, mama yangu anaingia vipi hapa?"

Jibu lake lilinishtua sana.

"Mtoto aliyezaliwa na wazazi wenye staha na yeye atakuwa kavaa vazi la staha la wazazi wake."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…