Wa...
Umeghadhibika.
Unawakebehi Waislam unasema,"Ahsante sana Mwl. Nyerere uliwaweza sana wadini hawa."
Ninì kimekukasirisha?
Kuwa Saigon wanasoma Khitma na kufuturisha kila mwaka?
Tuje kwenye tuhuma yako ya udini.
Nini ambacho wewe unaona katuweza?
Wazee wetu hawakuwa wabaguzi wa kumbagua mtu kwa dini yake.
Bahati mbaya Mwalimu yeye mwenyewe hakupenda kueleza historia yake ni vipi na ni nani waliompokea Dar es Salaam.
Bahati mbaya Mwalimu hakupata kueleza ni vipi alichaguliwa katika nafasi ya juu kabisa katika TAA katika uchaguzi wa mwaka wa 1953.
Mwalimu hakueleza kuwa ilikuwa shida kubwa kwake kushinda uchaguzi ule ambao alishinda kwa kura chache sana.
Ipo sababu yake ukitaka kujua niambie.
Mwalimu hakueleza hata kama alipata kugombea nafasi ya Rais wa TAA katika Ukumbi wa Arnautoglo dhidi ya Abdulwahid Sykes aliyekuwa Kaimu Rais wa TAA na Katibu; Katibu kwa miaka minne mfululizo kuanzia 1950 na Kaimu Rais kuanzia 1951.
Uchaguzi huu ulifanyika tarehe 17 April 1953.
Judith Listowel kaueleza vizuri uchaguzi huu katika kitabu chake, "The Making of Tanganyika," (1965).
Mimi nayajua mengi kupita Listowel kwa kuwa historia hii ni ya watu wangu ni historia ya wazee wangu na katika kuieleza si kuwa nataka kumueleza Nyerere la hasha Mwalimu anaingia kama sehemu ya historia ya wazee wangu.
Ushajiuliza kwa nini Nyerere hakupenda kueleza historia yake?
Ukitaka kujua nifahamishe.
Hawa wazee wangu ndiyo waliomuweka Nyerere madarakani na kumfikisha pale alipofika.
Kuwa wewe unathubutu kuwatusi wazee wangu na kuwaita, "wadini hawa," mimi sina la kukujibu ila neno moja tu kuwa "hutujui."
View attachment 1873424
View attachment 1873437
View attachment 1873457
Ndugu yangu,
Mtafute Julius Kambarage Nyerere katika makundi haya ya Waislam.
Picha ya juu mwaka ni 1956 watu wamerudi Hija wako shambani kwa Sheikh Abdallah Chaurembo Mtoni wamekusanyika kuomba dua kwa mengi na kubwa Tanganyika ipate uhuru.
Picha inayofuatia ina maelezo ni mwaka wa 1957.
Wako wapi hao Wengine?
(Wengine nimeweka herufi kubwa usidhani nimekosea ipo maana hapo).
Ikiwa hujui niulize.
Unajua sababu gani Wengine walikuwa wanamnyanyapaa Nyerere?
Ukitaka kujua sababu nifahamishe.
View attachment 1873454