Muuza Viatu,
Nilijua wasomaji wangu hawatashindwa kukitegua kitendawili hiki.
Lakini yako mengi yaliyopitika ukipenda unaweza kuita, "usaliti," la unaona hilo neno zito sana unaweza kujiridhisha kwa kusema ule ulikuwa mchezo wa siàsa.
Ilikuwaje "vijana wa mtandao," wakapoteza mechi katika kupiga zile penalti tano tano?"
Hivi karibuni Kikwete alisikika akisema kuwa iko siku ataeleza kwa nini aligombea urais.
Ningekuwa sikijui kisa ningeshangazwa na kauli hii.
Ningejiuliza kwani vipi kipi kinamfanya leo atake kumtoa paka ndani ya kapu?
Jambo si lishapita na watu tumesahau?
Ila namsifu Kikwete na Mtandao kwa kitu kimoja kuwa mwisho wa siku walichukua kikombe.
Salim Ahmed Salim alijaribu lakini aliposhindwa hakurejea tena ulingoni.
Kuna gazeti lilisema kuwa alishiriki katika kumuua Karume na pia siku nyingi ilikwishasemwa kuwa ni Muarabu.
Mara ya kwanza kukutana na Salim nyumbani kwake nilimuuliza kuhusu kuandika kumbukumbu zake.
Napitia kumbukumbu za Mzee Mwinyi labda nitaliona hili la Salim.
Halipo.
Katika kitabu chake Mzee Mwinyi kampamba sana Baba wa Taifa.
Sasa hapa nikajiuliza kwa nini kafanya vile?
Mzee Mwinyi alikuwa na tui mkononi asipolienga linaweza likakatika na yeye anazijua sheria za mchezo.
Kikwete katika hotuba yake ya kwanza Kibaha anagombea urais alilipamba Kanisa Katoliki kwa kusema kama si wao kumpa elimu angekuwa anakimbiza mabasi Chalinze huku ana kikapu cha karanga kichwani anawauzia abiria kwenye mabasi.
Kikwete na yeye pia alikuwa na tui mkononi.
Hizi ndizo sheria za mchezo huu.
Hautaki ujifanye mjuaji sana.
Ujue wapi kwa kuponda wapi na kwa kusifia.
Kikwete alikuwa na Prof. Malima katika kundi la wagombea wa CCM.
Kulikuwa na kichekesho au unaweza kuita, "tragic comedy," kilichoanzishwa na gazeti moja lililoandika kuwa, "Waislam Waiogopa Ikulu."
Sababu ya maneno haya ni kuwa hadi wakati ule hapakuwa na Muislam yeyote aliyejitokeza kuomba nafasi ya Urais.
Wahariri hao hao wakaja na lingine jipya ikasemwa kuwa wananchi Waislam wamekamia kuchagua rais Muislam.
Bunge likawaka moto.
Huko ni kuchanganya dini na siasa.
Mwiko mkubwa.
Ikabidi Waislam ndani ya Bunge kwa Spika waorodheshe majina yao kukataa kuwa wao wana nia ya kugombea urais.
Kikwete jina lake lilikuweko kwenye orodha ile.
Karatasi ilipofika kwa Prof. Malima msomi wa Princeton University, New Jersey yeye alikataa hata kuigusa ile karatasi.
Mzee Mwinyi kamtaja Prof. Malima katika hili sakata la uchaguzi wa mwaka 1995.
Lakini kwa ajili ya utu uzima mengi muhimu nadhani kasahau kuhusu Prof. Malima hivyo hakuyaandika.
Kasahau na haya ninayoeleza hapa hayamo katika kumbukumbu zake.
Laiti angeyakumbuka kitabu chake kingenoga sana.
View attachment 1877064
View attachment 1877065
View attachment 1877066