Ewe binti, ewe dada..chondechonde

Juandeglo

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2014
Posts
1,040
Reaction score
2,806
Habari zenu wakuu..

Leo naomba niongee na wewe binti, dada au hata mama unaweza kumwambia binti yako. Dunia ya leo ni dunia ya kizazi kilichoharibiwa na shetani. Malezi yamekuwa mabovu kwa sababu ya ubusy wa maisha. Unakuta mtu single mama inabidi apambane kwa ajili ya mtoto wake ale, avae.. hapohapo kuna muda anaweza pata ashki atafanyeje inabidi sometimes jirani aachiwe mtoto yeye akazitulize kwa "uncle"

Ok..am not condemning anybody. Iko hivi. Kama unaingia kwenye ndoa ingia na mentality hii. Furaha yako isitoke kwa huyo bwana na hata mwanaume furaha yako isiwe kwa huyo mwanamke.(najua wanaume watasoma pia). Wote tujitahidi furaha zetu zitoke kwa kumcha Mungu. Wewe mwanaume unapotumikia kusudi lako hapa duniani..kwa uaminifu basi ndipo ufurahi. Ni mtego kutegemea mwanadamu ambae si malaika akupe furaha.

Unakuta mwanamke umeolewa, ukazaa watoto wanne afu mwanaume yuko busy na wengine huko nje tena yumkini akaleta na watoto...kama huna Mungu moyoni kila kitu kitavurugika. Wanawake huwa mnasacrifice vingi sana kwa ajili ya wenza na bado matukio mnapigwa. Wanaume naturally ni wabinafsi. Ubinafsi wao unawakandamiza na kuwaumiza nyinyi.

Kama wewe ni mwanamke na bado hujaingia ndani ya ndoa, kuwa na ujuzi. Hata kazi kama hujapata ila ujuzi utakupa faida na kukuingizia pesa. Ujuzi utakuweka busy..hutagusa simu ya mtu(for your own happiness), hutauliza maswali ya chokochoko, hutasumbuana na mtoto wa mama mkwe. We utakuwa busy na kulea plus biashara zako, tuone kama utaumia. Ukimtegemea mwanaume akupe furaha asilimia mia utatubu...hawana muda.

NB: hata unapokuwa busy mume anabaki palepale..usimnyime, mjali, muheshimu na kumtii, afu usimfatilie hata...kama ni maswali ya kuchelewa kurudi muulize lakini kwa hekima na adabu..na ukiona mgogoro shuka chini, au kama unaweza amka usiku piga magoti kemea hayo mapepo..utaona. Kama mwanamke unajielewa na ukafanya haya kama akiamua kucheat ni yeye na anayoyatafuta atayapata hakika.

Naongea haya kwa kukujali na kutamani kuona furaha yako wewe dada yangu.
 
Andiko zuri sana.

Wosia safi.

Ndiyo. Hakuna mwanaume mkorofi mbele ya mwanamke mwenye busara na hekima. Mwanamke anayejua wapi ajishushe na wapi agangamare. Anayejua mipaka yake. Ni mwanaume gani atafurukuta mbele ya mwanamke anayejua kuwa mumewe ni kuhani, mlinzi na kichwa cha familia?

Shida ni hivi vibinti visomi hivi vinavyojifanya kujua kila kitu viingereza vingi mpaka puani na ufeminist usio na kichwa wala miguu. Kila siku makelele tu ndani ya nyumba kimeshaota mapembe mpaka mwanaume unaiogopa nyumba uliyoijenga mwenyewe 🚮🚮🚮🚮

Again andiko zuri sana. Litawasaidia mabinti wenzio (kama watalizingatia) 👏👏👏👏
 
Furaha Yako isipotoka Kwa mkeo au Kwa mumeo umeingia kwenye ndoa kufata Nini?

Unless kama unataka kusema watu wasioe Wala kuolewa. Ndoa ni zaidi ya tendo la ndoa na kama hitaji ni tendo la ndoa tu mbona yanapatikana mengi tu nje huko, ila je ndio dhamiri za mahusiano hizo?


Usipopata Furaha Kwa mumeo au mkeo utaipata na kuitafuta Kwa mchepuko.
 
Asante kwa mtazamo wako mkuu. Lakini unafikiri ndoa ni furaha kila siku. Hujui kama ndoa ina majira. Mungu tu alieumba dunia aliweka majira makusudi ndo itakuwa ndoa.

Watu waingie kwenye ndoa wakijua pia shida, tabu, mateso yapo. Kama kusingekua na mateso tusingeapa katika shida na raha. Shida ziko palepale. Aliye single na aliye kwenye ndoa wote wana tabu tu.

Ukiwa hujaolewa utachezewa na karaha za kutokupewa pesa mpaka uvue chupi. Ukiolewa mtu anaweza achelewe kurudi au hata kakasirishwa huko atokako labda ni kazini lakini joto ukalionja wewe.

Duniani dhiki tu furaha mbinguni. Kama mtu hana utayari na ukomavu wa moyo kuingia kwenye ndoa na asiingie. Kwa sabbu tabu iko palepale. Ndugu tu nyumbani kuna misuguano ndo mtu mliekutana nae utu uzimani. Marriage aint a joke..huo ndo ukweli.

Bado dada hujakutana na mwanaume tayari alishazaa watoto wawili nje afu we ndo unachaguliwa kuolewa na hao watoto ukae nae. Imagine uchelewe kupata mtoto, afu bado unawalea hao. Ukiwafinya au kuwakanya unashangaa mawifi, mama mkwe au hata mama za hao watoto wanakusakama "au kisa hujazaa". Hata kama watoto unawalea kwa upendo. Tena na matusi juu. Na wewe umewapenda na kuwalea vizuri tu. Au yumkini watoto wengine wamepatikana ndani ya ndoa. Mme katika tembea tembea kakuletea hao apo. Na unatakiwa unyamaze tena ulee kana kwamba ni wa kwako. Bila strong mentality hakika utafia jangwani mpendwa. Kweli nakwambia.

Vidada vya siku hizi blue tick tu roho inataka kukutoka shosti. Unaanza kuona hupendwi. Na hivyo mamotiveshen spika walivyojaa. Unakutana na meme "hakuna mtu anaekosa muda kwa mpenzi wake". Shoga unaibeba jumlajumla unaanza kuona huyu hanipendi. Unamuacha na hapo kashakukula sana. Mwanaume hana cha kupoteza. Wewe sasa. Ndo unajikuta muda unaenda tu. Kisa mind games. Blue tick tu...roho juu. Je akirudi saa tisa usiku utahema wewe. Asiporudi siku tatu je..naongea na wewe dada angu. Jipange sawasawa dunia ishavaa chupi. Kula vizuri..ridhika, fanya kazi hata upate 5000 yako tu kwa siku, ishi maisha ya level yako sio social mediaz(usione wenzako vikoba na wewe umo) kumbe huna uwezo. Utat***wa sana nje. Sali sana, toa sadaka, penda sana(upendo) then funga pia, fanya mazoezi...jiweke busy, akili yako ishughulishe..kamwe hutateseka dunia hii. Ila ukikaa kumchunga mtu mzima...heheee
 
Mnanichanganya wakuu navurugika haswaaaa!

Kwenye kikao cha wanaume tulisema wanawake ni wabinafsi lakini huku tena nakuta wanaume ni wabinafsi, hapo ndo mkanganyiko uliopo

Nani ni yupi na yupi ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mimi mapenzi yamenishinda naona kabisaaa
 
Mwanamkeee kwangu mm n chomombo cha stareheee km ilivyo pombe na marijuana ilaa c ktu chakusema niishii nikiwaziee kinipe stress, mbona

YESU christo aliishii bila dem na mkee, mm Ninani nioee
 
KWENYE KIAPO CHA NDOA, KUNA MANENO KWA 'SHIDA NA RAHA'
SHIDA SIO ZA UCHUMI AU UGONJWA PEKEE, TOFAUTI ZA MALEZI NA MAKUZI NI TATIZO BILA UVUMILIVU. NDOA INAKUWA NGUMU SANA.
 
Mnanichanganya wakuu navurugika haswaaaa!

Kwenye kikao cha wanaume tulisema wanawake ni wabinafsi lakini huku tena nakuta wanaume ni wabinafsi, hapo ndo mkanganyiko uliopo

Nani ni yupi na yupi ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wote ni wote na chote ni chote mkuu. Aahrghh we vurugika tu.

Mada nzuri mleta uzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…