Ewe mjasiliamali ifanye siku yako kuwa nzuri ukuamka asubuhi wajulie hali wanaokudai

twijuke

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
547
Reaction score
252
Kama mjuavyo ni nadra sana kukuta mjasiliamali si mdeni, mfumo wa shuguli za biashara au uzalishaji mali unapelekea watu kuwa na madeni. Imefika mahali mtu anaogopa kupokea simu kwa namba ngeni huku akidhani huenda anayemdai kaamua kutumia namba nyingine. Hali hii imepelekea kupunguza ufanisi wa utendaji kazi.

Yawezekana mtu anaye kupigia anataka akupe order ya bidhaa unazouza au kusindika, lakini wewe unaogopa kupokea ukidhani ni simu yenye mahusiano na madeni. Ushauri wangu ukiamka asubuhi kama mfanya biashara au mjasiliamali, jambo la kwanza ni kuitengeneza siku, katika kuitengeneza siku iwe ni pamoja na kuwajulia hali wanaokudai, kufanya hivi inakuweka kwenye nafasi nzuri kama mjasiliamali au mfanya biashara namna ya kuratibu mambo yako kutwa nzima, kwani kutwa utapokea simu zote pasipo hofu. Tuseme ukweli kwamba uongo garama yake ni kubwa kuliko ukweli, ndo maana wanasema "kweli utakuweka huru daima".
 
Kabla hatujaenda mbali aisee naomba ufafanue hapo namna ya kutengeneza siku asubuhi, una maana gani
 
unadaiwa halafu huna hela ya.kulipa deni hiyo siku unaitengenezaje mkuu?
 
Back
Top Bottom