Ewe Mtanganyika, ukimsikia Mtawanyika akisema hakuna Mungu, wala sala hazisaidii, mtizame usoni kisha utabasamu na uondoke zako.

Ewe Mtanganyika, ukimsikia Mtawanyika akisema hakuna Mungu, wala sala hazisaidii, mtizame usoni kisha utabasamu na uondoke zako.

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
529
Reaction score
1,150
Wanajukwaa

Kuna changamoto moja ya kiafya ilinipiga - yaani ilikuwa mwili nauhisi kabisa upo na shida ila nilivyoenda hospitali kama mara tatu kwa vipimo nikaambiwa sina shida yoyote.

Ile hali ikawa inapelekea mimi kuwa mtu wa kulala lala tu, kazi zangu nazifanya kivivu, na kibaya zaidi nikakosa na hamu ya kula hivyo mwili dizaini kama ukakata ringi, na nikawa pia nina mawazo na stress kimtindo. Na kuna michongo yangu kama miwili ikawa nayo dizaini imekwama.

Mimi kwa dini ni mkatoliki, ila ni wale wakatoliki jina tu, jumuiya siendi wala kanisani siendi (japo wazazi wananiambia nilitabiriwaga kuwa padri nikiwa mdogo na hata mafundisho nilikuwaga mtu wa kwanza kabisa).

Hivyo ikabidi usiku mmoja kabla ya kulala, nikasema leo nitamkumbuka Mungu, kwahiyo kwakuwa mimi sio mtu wa kujua sala, nikasema kwakuwa mimi ni Mkatoliki nitatafuta Novena nisali. Nikapekua mtandaoni nikaona Novena ya Mt. Ritha Kashia, nikajisemea nitakuwa naisali hii sala kila usiku kabla ya kulala.

Ilikuwa ni terehe 5 ya January ndipo nilipoanza na nilisali mpaka usiku wa tarehe 13. Nilivyolala siku hiyo, kesho yake tarehe 14 kulikuwa na kikao kazini hivyo nikawapia nimejiandaa kwa kikao.

Hiyo siku ya tarehe 14 naweza kusema ndo ilikuwa siku ya kupokea miujiza yangu, na ilikuja baada ya mimi kuzimia ghafla kwenye kikao nikiwa najiandaa kuchangia hoja ya mwenyekiti.

Kuzinduka nilikuwa hospitalini, na nikaja kuambiwa na daktari kwamba nilikuwa nina uchovu, mwili kukosa maji, sukari ilikuwa chini etc.

So dozi ikawa ni ile drip na ushauri wa kuzingatia unywaji wa maji na misosi. Kwahiyo ikawa hivo pale hospitali ambapo walikaa na mimi kama siku tatu hivi wakinipima lakini hawakuona ugonjwa.

Baada ya kutoka hospitali naweza kusema ndo ikawa kama nimefungu ukurasa wa kuishi upya baada ya miezi takribani 4 isiyojulikana.

Nimepata recovery kubwa mno na ya haraka na nguvu ya kazi imerudi maradufu.

Ni baada ya kutafakari mwenendo wa matukio yote ndipo naona kabisa kuna vitu visivyo vya kawaida; japo huu sio uzi wa kuyathibitisha yasiyo ya kawaida bali ni kuutukuza ukuu wa Mungu pale unapomkumbuka kwa maombi.

Kwa sasa nipo nimevaa rozari masaa yote na nimeamua sasa kwamba nitamtumikia Mungu kwa moyo mmoja kwa kusali na kuendeleza yaliyo mema kwakuwa nimeona muujiza wake, halikuwa tendo rahisi lile la tarehe 14 (siku takribani nane au kumi baada ya kuanza maombi).

Hivyo kwa sasa, nikisikia mtu anasema hakuna Mungu na hizi sala na maombi ni ubatili mtupu, mimi nitamtizama usoni na kutabasamu, kisha nitaondoka zangu.

Good Morning
 
....hoja nyepesi sana hii.
haiwezi kutetea jambo tata kama la Mungu hii issue yako.
 
Hukufunga Kwa Iman kwanini uzimie Kwa kukosa sukari?
 
Back
Top Bottom