tethering
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 331
- 139
Hivi ewra mana mfumo wa kupima ubora nishati ya mafuta yanayotumiwa na vyombo vya moto kutoka vituo vya kuuzia mafuta maeneo yote hapa Tanzania? Kama hamna utaratibu huo naomba muwe mnafanya hivyo tafadhari, napata shaka sna unakuta petrol inanuka mafuta ya taa kabisa tofauti na nilivyozoea,nimezoea petrol ukiipaka sehemu kidogo ni sekunde chache imekauka,sasa Wakati mwingine inachelewa utadhani umepaka maji, siku moja niliweka mafuta petrol kiasi kwenye kituo fulani mkoa fulani mara baada ya kutoka pale chombo kikawa kinazima zima mara kwa mara baadae nikaenda kituo x nikachanganya(dilute) na yale chombo kikaacha kuzimazima. Nahii imekuwa ikijitokeza maeneo mengi. Tusaidieni kulinda ubora wa nishati hiyo kwa mlaji. Itapelekea kulinda vyombo vya moto na uchumi pia.Asante