EWURA: Bei ya Mafuta itaendelea kupanda

EWURA: Bei ya Mafuta itaendelea kupanda

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa kutokana na uhitaji mkubwa wa mafuta, bei ya yake inatarajiwa kuendelea kupanda zaidi hali inayochangiwa na vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, huku usafirishaji na upokeaji wake nchini kuwa hafifu.

Akizungumza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Godfrey Chibulunje alipokuwa katika mdahalo uliohusisha Wahariri na waandishi wa habari hapo alisema kuwa, mfumuko wa bei unasababishwa na changamoto mbalimbali inayoikumbuka miundombinu ya usafirishaji kutoka na sababu za kivita.

Alibainisha kuwa katika soko la dunia bei ya mafuta imepanda kwa kiasi kikubwa, huku akieleza kuwa mwezi Desemba 2021 tani moja ya mafuta ya petroli ilikuwa inauzwa dola 717, na hadi kufikia Machi, 2022 ilipanda hadi kufikia dola 1,106 kwa tani moja.

"Bei za mafuta zinatofautiana sana katika maeneo mbalimbali duniani, barani Afrika, Ulaya na Amerika, wakati Tanzania lita moja ya dizeli ikiwa inauzwa TZS 2,403, Kenya ni 2,331 na Uganda 2,830, hivyo ukiangalia nchini kulikuwa na unafuu kwa kiasi fulani,” amesema.

Aidha, aliongeza kuwa kesho watatangaza bei mpya ya mafuta na mara baada ya vita kuisha hali itarudi kuwa shwari.

Chanzo: Swahili

Soma---
EWURA: Hifadhi ya Petrol ya iliyopo Tanzania ni ya siku 27, jiandaeni kwa bei mpya Jumanne Aprili 5, 2022
 
Mungu tupe nusra.
notagain1.png
 
Mafuta lita moja ni 15,000/- Zimbabwe
 
Tuuzeni nchi tugawane hela au mnasemaje..

Naomba niulize hivi hakuna nchi nyengine ambapo tunaweza kupata mafuta kwani lazima urusi tu..?
 
Ndio tutumie akili zetu kubuni njia mbadala ikiwemo magari ya umeme haswa umeme jua, kuboresha usafiri binafsi ili watu wasiendeshe magari yao sana...
 
Hawa jamaa et baada ya vita kuisha..[emoji849][emoji849]
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa kutokana na uhitaji mkubwa wa mafuta, bei ya yake inatarajiwa kuendelea kupanda zaidi hali inayochangiwa na vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, huku usafirishaji na upokeaji wake nchini kuwa hafifu.

Akizungumza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Godfrey Chibulunje alipokuwa katika mdahalo uliohusisha Wahariri na waandishi wa habari hapo alisema kuwa, mfumuko wa bei unasababishwa na changamoto mbalimbali inayoikumbuka miundombinu ya usafirishaji kutoka na sababu za kivita.

Alibainisha kuwa katika soko la dunia bei ya mafuta imepanda kwa kiasi kikubwa, huku akieleza kuwa mwezi Desemba 2021 tani moja ya mafuta ya petroli ilikuwa inauzwa dola 717, na hadi kufikia Machi, 2022 ilipanda hadi kufikia dola 1,106 kwa tani moja.

"Bei za mafuta zinatofautiana sana katika maeneo mbalimbali duniani, barani Afrika, Ulaya na Amerika, wakati Tanzania lita moja ya dizeli ikiwa inauzwa TZS 2,403, Kenya ni 2,331 na Uganda 2,830, hivyo ukiangalia nchini kulikuwa na unafuu kwa kiasi fulani,” amesema.

Aidha, aliongeza kuwa kesho watatangaza bei mpya ya mafuta na mara baada ya vita kuisha hali itarudi kuwa shwari.

Chanzo: Swahili

Soma---
EWURA: Hifadhi ya Petrol ya iliyopo Tanzania ni ya siku 27, jiandaeni kwa bei mpya Jumanne Aprili 5, 2022
EWURA wao wanatekeleza maagizo ya mwenye nchi keshasema lazima mafuta yapande bei na bidhaa zingine.
 
Back
Top Bottom