EWURA: Bei ya Mafuta itaendelea kupanda

EWURA: Bei ya Mafuta itaendelea kupanda

Angeshusha mafuta ya kula tuweze kupika hata japo matembele yanayo ota chooni
 
Tungejikita kuwekeza kwenye gesi yetu leo tusingekuwa na shida kama hii, kiburi alichonacho urusi ni rasilimali ya gesi na mafuta tu baasi.
 
Waache uongo wakanunue mafuta Urusi. Urusi inauza kwa punguzo la bei hadi 25% sasa kwanini wameng'ang'ania kununua ya bei ya juu? Waache kujificha kwenye vita ya urusi-ukraine



 
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa kutokana na uhitaji mkubwa wa mafuta, bei ya yake inatarajiwa kuendelea kupanda zaidi hali inayochangiwa na vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, huku usafirishaji na upokeaji wake nchini kuwa hafifu.

Akizungumza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Godfrey Chibulunje alipokuwa katika mdahalo uliohusisha Wahariri na waandishi wa habari hapo alisema kuwa, mfumuko wa bei unasababishwa na changamoto mbalimbali inayoikumbuka miundombinu ya usafirishaji kutoka na sababu za kivita.

Alibainisha kuwa katika soko la dunia bei ya mafuta imepanda kwa kiasi kikubwa, huku akieleza kuwa mwezi Desemba 2021 tani moja ya mafuta ya petroli ilikuwa inauzwa dola 717, na hadi kufikia Machi, 2022 ilipanda hadi kufikia dola 1,106 kwa tani moja.

"Bei za mafuta zinatofautiana sana katika maeneo mbalimbali duniani, barani Afrika, Ulaya na Amerika, wakati Tanzania lita moja ya dizeli ikiwa inauzwa TZS 2,403, Kenya ni 2,331 na Uganda 2,830, hivyo ukiangalia nchini kulikuwa na unafuu kwa kiasi fulani,” amesema.

Aidha, aliongeza kuwa kesho watatangaza bei mpya ya mafuta na mara baada ya vita kuisha hali itarudi kuwa shwari.

Chanzo: Swahili


Soma---
EWURA: Hifadhi ya Petrol ya iliyopo Tanzania ni ya siku 27, jiandaeni kwa bei mpya Jumanne Aprili 5, 2022
Maushungi alishapigilia msumari
 
Wakimaliza kupandisha mafuta wapandishe na majini[emoji23][emoji23]
 
Tuuzeni nchi tugawane hela au mnasemaje..

Naomba niulize hivi hakuna nchi nyengine ambapo tunaweza kupata mafuta kwani lazima urusi tu..?
Baada ya hii vita ndio nimejua mafuta yanatoka huko siku zote niliaminishwa mafuta yanatoka kwa mwarabu
 
Dikteta lazima asakamwe na kila mwenye akili timamu
Wewe na rais wako wote hamjielewi.kufanya hivyo ndo kutapunguza ukali wa maisha kwa wananchi wake!??utimamu wako wa akili uko wapi kama unavyo jinasibu!? Jinga mmoja
 
Back
Top Bottom