Nchi za kiarabu kwa muda mrefu zilikuwa zikitumia mafuta kama kombora lao la kivita.Miaka ya nyuma walikuwa wakitumia mafuta kugomea kuwauzia mafuta wale ambao hawataki kuwaunga mkono waarabu au wapalestina au wale ambao walikuwa na uhusiano wa Kibalozi na Israeli.Ilikuwa ukikataa kuwaunga mkono wanakunyima mafuta.
Tanzania chini ya Nyerere ilijikuta ikilazimika kuvunja uhusiano na Israeli kwa shingo upande kwa kulazimishwa ili iweze kuendelea kupata mafuta toka nchi za kiarabu.Ndiyo maana kipindi kile Nyerere akajifanya kinara wa kuunga mkono wapalestina na kundi lao la PLO.
Mapesa ya mafuta toka uarabuni pia yamekuwa yakituhumiwa kutumika kufandhili makundi ya magaidi kama Hamas,hizbollah,n.k katika nchi mbalimbali na makundi yaliyolipua Trade centre marekani, balozi mbalimbali za Marekani na mataifa mengine,n.k Pia mapesa hayo ya mafuta yamekuwa yakitumika kugharimia vikundi vyenye imani za itikadi kali vinavyoleta shida na mauaji katika nchi mbalimbali dunian ikiwemo Pakstani,Bali,uarabuni,Misri,Africa,n.k
Ili kupambana na vita ya kutumia mafuta mbinu kadhaa zimebuniwa na makomandoo wa vita za uraiani zisizohusisha vita za silaha za moto.Mojawapo ya silaha hiyo ni kuhakikisha kuwa mafuta yanatafutiwa teknolojia mbadala ili kuyafanya yasiendelee kuwa na soko na kupunguza jeuri ya waarabu kuitumia silaha hiyo.Baaddhi ya Mbinu hizo ni kama:
(a) Ugunduzi huo ni pamoja na kutumia mimea mbalimbali ya kuzalisha mafuta ikiwemo mbono,n.k
(b) Pia magari na mitambo ya viwanda kutengenezwa inayotumia gesi ambayo tayari imeshaanza kufanya kazi hata Tanzania viwanda vimeanza kutumia gesi badala ya songosongo badala mafuta ya waarabu.Magari mengi muda si mrefu yatakuwa yakitumia gesi zaidi badala ya mafuta ya waarabu
(c) Kuachilia teknolojia ya ugunduzi wa mafuta holela ili kila nchi iweze kufanya utafiti wake na kuona kama inayo mafuta na ikiyaona iweze kuyachimba na kuacha kutegemea waarabu.Tanzania na hata Pemba mafuta yapo nadhani muda si mrefu hatutakuwa na la kujikomba kwa waarabu tutawaachia mafuta yao wayanywe wakitaka kwani tutachimba yetu.
(d) Nchi kubwa kama marekani N.K kuacha kuagiza mafuta kutoka uarabuni na kuanza kutumia reserve zake na kuchimba yake kumeleta pigo kubwa la ajabu kwa waarabu ambalo limesababisha bei ya mafuta kuporomoka kwa kasi ya kutisha hadi Tanzania.Bush kawashikisha adabu waarabu Marekani mnunuzi mkubwa wa mafuta kawapiga chini sasa waarabu wako tayari kuuza kwa bei ya kutupwa mafuta yao na bei yao itaendelea kuporomoka .Wauza mafuta wameanza kugeuka kama machinga wanahaha kusaka soko kuuza mafuta popote kwa bei za kutupwa.Mapipa na mapipa yameanza kujazana kwenye maghala yao bila wanunuzi.
Vita hii ya mafuta ni kali. Inavyoelekea miaka michache ijayo Uarabuni litakuwa bara maskini kuliko yote.Watakuwa maskini kuliko hata bara la Afrika sababu wao hawalimi,hawajaendelea kiviwanda,teknologia wala madini. Tegemeo lao ni silaha ya mafuta tu ambayo sasa inapigwa makombora ya nguvu kuisambaratisha silaha hiyo
Muda si mrefu waarabu wataiheshimu Afrika na watakuja na bakuli la kuomba kama la omba omba Matonya yule ombaomba maarufu kuja kutuomba misaada tuwasaidie walau chakula wale.
Watanzania tujipange tuimarishe na kuijali sekta ya madini,kilimo na viwanda tutafika mbali sana muda si mrefu tukichachamaa na viongozi wakijipanga vizuri kujali maslahi ya nchi na wananchi ili raslimali zilizopo zisimamiwe vizuri kwa maslahi ya wananchi tutafika mbali.
Mafuta ya waarabu ni bomu ambalo halitakuwa na nguvu yoyote ya kumtisha yeyote muda wa miaka michache tu ijayo.Tanzania tutakuwa huru hata twaweza kulala na kuamuka TEL AVIV ISRAEL bila kuogopa muuza kombora la mafuta mwarabu anasemaje au anatuwazia nini kwa sababu atakuwa muuza kombora lisilolipuka lisiloweza kulipua hata inzi mdogo.