BUBE
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 845
- 254
Ni Siku ya pili leo tangu ipite ile tarehe tuliyoahidiwa kupata neema ya punguzo la bei ya mafuta. Ni jambo la kuchefua kuona kuwa, mara tu baada ya serikali kutangaza kupitia kwa waziri wa fedha kuhusu kodi za mafuta. Jambo linalosikitisha na KUNITIA WAZIMU ni kwamba tarehe mosi Julai wauzaji wa mafuta walipandisha bei ya mafuta ya taa! Sina hakika kama hawa wauzaji walikuwa wameingiza consignment iliyotozwa kodi mafuta ya taa kulingana na bajeti ya mwaka 2011/12. Sasa hadi leo hii inashangaza kuona kuwa wauzaji hao hawajapunguza mafuta ya petrol na diesel. Swali la msingi hapa ni je EWURA, TRAs na serikali kwa ujumla hawaoni huu ni uhuni? Angalizo: Mods tafadhali msiitoe hii topic