EWURA wanatekeleza miradi gani ya maendeleo hapa nchini

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
EWURA- Energy and Water Utilities Regulatory Authority na kwa kiswahili ni Mamlaka ya uthibiti ya Nishati na Maji kila malipo ya huduma hizo kutoka kwa watumiaji wote inakusanya 1% kama tozo. Hizi ni fedha nyingi sana na hasa ukizingatia uwingi wa watumiaji wa umeme, gesi na maji.

Aidha EWURA ni miongoni mwa taasisi chache za umma ambazo zinalipa mishahara mikubwa kwa watumishi wake. Ni vizuri kulipa mishahara mizuri kwa watumishi lakini pia ni vema mishahara mikubwa iendane na huduma na uwekezaji katika maendeleo ya nchi ili kupunguza makali ya maisha magumu ya wananchi.

Binafsi sifahamu mradi wo wote wa maendeleo unaotekelezwa na EWURA. Ningependa nifahamishwe je fedha zote za tozo zinazokusanywa ni kwa ajili ya mishahara, mafunzo na posho za safari tu? Nakumbuka enzi za Magufuli EWURA ni miongoni mwa taasisi za umma zilizolazimishwa kutoa gawio kwa serikali, je mpaka leo gawio linatolewa?

Isije ikawa EWURA ni tobo la kuvujisha fedha za umma!
 
Ni kweli tozo ya 1% ni kubwa mno kwa taasisi ndogo kama EWURA, ni busara ikashushwa hadi angalau 0.5%.
Ni kama CWT tu. Wanapiga kila mwezi 2% za walimu wa serikali nchini, halafu 90% ya hizo hela wanaishia tu kulipana posho na mishahara! Huku walimu wakiendelea kudharauliwa mtaani mpaka na laymen.
 
Ada zote zinazotozwa na vyama vya wafanyakazi ni wizi mtupu kwa sababu hakuna msaada wo wote vyama hivi vinatoa!
 
Taasisi nyingi za serikali zimeundwa kwa lengo la kuwaibia wananchi, halafu mwisho wa siku hizo hela za dhuluma wanaishia tu kulipana posho na mishahara minono.
Tuliza wenge. Njoo tufanye umachinga hapa Ilala
 
EWURA- Energy and Water Utilities Regulatory Authority na kwa kiswahili ni Mamlaka ya uthibiti ya Nishati na Maji kila malipo ya huduma hizo kutoka kwa watumiaji wote inakusanya 1% kama tozo. Hizi ni fedha nyingi sana na hasa ukizingatia uwingi wa watumiaji wa umeme, gesi na maji.

Aidha EWURA ni miongoni mwa taasisi chache za umma ambazo zinalipa mishahara mikubwa kwa watumishi wake. Ni vizuri kulipa mishahara mizuri kwa watumishi lakini pia ni vema mishahara mikubwa iendane na huduma na uwekezaji katika maendeleo ya nchi ili kupunguza makali ya maisha magumu ya wananchi.

Binafsi sifahamu mradi wo wote wa maendeleo unaotekelezwa na EWURA. Ningependa nifahamishwe je fedha zote za tozo zinazokusanywa ni kwa ajili ya mishahara, mafunzo na posho za safari tu? Nakumbuka enzi za Magufuli EWURA ni miongoni mwa taasisi za umma zilizolazimishwa kutoa gawio kwa serikali, je mpaka leo gawio linatolewa?

Isije ikawa EWURA ni tobo la kuvujisha fedha za umma!
Umesema mwenyewe ewura ni mamlaka ya kudhibiti nishati na maji,
Haizalishi kitu, ni kama refa,haichezi ni kusimamia wachezaji kwenye sekta hiyo.
Ni sawa na polisi, takukuru, miradi wanayoweza kufanya ni soft type, programs,
 
Sawa! Kwa nini sasa watoze tozo kubwa kiasi hicho wakati kwanza ni wachache na pili kazi zao ni soft component?
 
EWURA- Energy and Water Utilities Regulatory Authority na kwa kiswahili ni Mamlaka ya uthibiti ya Nishati na Maji kila malipo ya huduma hizo kutoka kwa watumiaji wote inakusanya 1% kama tozo. Hizi ni fedha nyingi sana na hasa ukizingatia uwingi wa watumiaji wa umeme, gesi na maji.

Aidha EWURA ni miongoni mwa taasisi chache za umma ambazo zinalipa mishahara mikubwa kwa watumishi wake. Ni vizuri kulipa mishahara mizuri kwa watumishi lakini pia ni vema mishahara mikubwa iendane na huduma na uwekezaji katika maendeleo ya nchi ili kupunguza makali ya maisha magumu ya wananchi.

Binafsi sifahamu mradi wo wote wa maendeleo unaotekelezwa na EWURA. Ningependa nifahamishwe je fedha zote za tozo zinazokusanywa ni kwa ajili ya mishahara, mafunzo na posho za safari tu? Nakumbuka enzi za Magufuli EWURA ni miongoni mwa taasisi za umma zilizolazimishwa kutoa gawio kwa serikali, je mpaka leo gawio linatolewa?

Isije ikawa EWURA ni tobo la kuvujisha fedha za umma!
Ileje mnasema uthibiti huku Dar tunasema udhibiti.
 
'Wanadhibiti' zile asilimia za fedha za watanganyika kwenye mafuta, umeme, maji, gesi n.k

Kazi yao ni kukusanya huo mpunga na kuenjoy maisha.
 
Back
Top Bottom