Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Maelekezo hayo yametolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile, wakati akifungua kikao kazi cha kuhakiki taarifa kwa watendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimidogo, jijini Dodoma leo, 30 Oktoba 2024.
Dkt. Andilile alisema kuwa, EWURA imetathmini taarifa zote zilizowasilishwa na Mamlaka hizo katika mfumo wa MajIs kwa Mwaka 2023/24 na kubaini takwimu zisizo sahihi za kiwango cha maji yanayozalishwa, muda wa upatikanaji wa huduma, usimamizi wa usafi wa mazingira,hali ya upatikanaji na kiwango cha uhitaji wa maji,ubora wa maji pamoja na upotevu wa maji.
“Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora ya maji na inayokidhi mahitaji yao ya kila siku, tunapokosa takwimu sahihi, ni ngumu kuwapatia wananchi huduma hiyo, hivyo mnatakiwa mtoe kipaumbele katika kuwasilisha takwimu na ziwe sahihi.
Mha. Jovitus Kichum, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, aliwasisitiza watendaji hao kuhakikisha takwimu zinazowekwa kwenye mfumo wa MajIs zinaakisi uhalisia ili Serikali iweze kutatua changamoto zinazojitokeza kwa lengo la kuimarisha huduma za majisafi na usafi wa mazingira nchini.
EWURA