EWURA yashusha Bei za Mafuta : Petroli Imeshuka Tsh 92, Dizeli Tsh 204 na Mafuta ya Taa Tsh 440

EWURA yashusha Bei za Mafuta : Petroli Imeshuka Tsh 92, Dizeli Tsh 204 na Mafuta ya Taa Tsh 440

Mimi naiomba EWURA, chonde chonde, fanya lolote uwezalo ili mwezi ujao bei ya petroli ifike Tsh 10,000/= kwa lita, ili tuone kama hawa wenye Vi-Toyota corolla au vi Passo sijui Carina namba A au B au C wataviingiza barabarani.

Hivi vigari vichafu chafu vinatujazia nzi na foleni huku Dar es aalaam.
 
Screenshot_20260805_180506_TradingView.jpg
bei kwa pipa $74 inazidi kushuka na leo trump na iran wanaendelea na mazungumzo
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza rasmi bei mpya kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini, zikionyesha nafuu kubwa kwa wananchi kuanzia LEO Jumatano, Tarehe 05 Agosti 2026 saa 6:01 usiku.


Katika mabadiliko hayo ya mwezi Agosti, bei za mafuta zimeshuka nchinzima kutokana na mwenendo wa bei katika soko la dunia:


Petroli: Imeshuka kwa TZS 92 kwa kila lita.

Dizeli: Imeshuka kwa TZS 204 kwa kila lita.

Mafuta ya Taa: Yameshuka kwa TZS 440 kwa kila lita.

View attachment 3643462View attachment 3643463
Kupanda ilipanda kwa Speed ya Jet ila kushuka inashuka kwa speed ya kinyonga.
 
Time to invest in electric cars, solar panels na battery storage kwenye nyumba zetu ili kuwakata hawa umbwa cartels na TANESCO, ukipiga hesabu vizuri utaacha kuwa mteja wao
 
Hivi kupunguza sh. 100 ama 90 unaweza kujigamba hadharani kwamba umepunguza bei ili kuboresha maisha ya watu na hatua kali zichukuliwe kwa watakaokaidi!

Ninacheka kwa kukenua meno bila bashasha huku uso umenuna kwa chuki.
Ni kwa kuwa we fukara mshamba huielewi biashara ya mafuta. Dizeli kushuka kwa sh 204 ni punguzo kubwa sana matajiri wanajua ila maskini km wewe utabaki ulivyo mpaka kiama
 
Kwenye kupanda ilijua 3500 hadi 4800 lakn kushuka ndo hizo mia kwanini wasishushe hata 500
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza rasmi bei mpya kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini, zikionyesha nafuu kubwa kwa wananchi kuanzia LEO Jumatano, Tarehe 05 Agosti 2026 saa 6:01 usiku.


Katika mabadiliko hayo ya mwezi Agosti, bei za mafuta zimeshuka nchinzima kutokana na mwenendo wa bei katika soko la dunia:


Petroli: Imeshuka kwa TZS 92 kwa kila lita.

Dizeli: Imeshuka kwa TZS 204 kwa kila lita.

Mafuta ya Taa: Yameshuka kwa TZS 440 kwa kila lita.

View attachment 3643462View attachment 3643463
Sas hapa wameshusha ama wameficha wizi🤔🤔
 
Sio haba maana itasaidia kidogo lakini bado mafuta yanatakiwa yashuke atlest 200 kwanini nasema hivyo kwenye mafuta kuna kodi/tozo za serikali zinaweza punguzwa na kuleta unafuu kwenye bidhaa ya mafuta
Kabisa mkuu maana wakishusha hata senti nakwambia watapiga domo balaa akati kupanda yanapanda hadi elfu kwa mara moja ila kushuka dah..!!
 
Wewe hata uharo unashangilia as long as umetoka kwenye hii serikali ya hovyo
Gentleman,
mihemko na makasiriko yako ni kwasababu EWURA wameshusha bei ya mafuta nchini au una chuki binafsi tu isiyo na sababu? :pedroP:
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza rasmi bei mpya kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini, zikionyesha nafuu kubwa kwa wananchi kuanzia LEO Jumatano, Tarehe 05 Agosti 2026 saa 6:01 usiku.


Katika mabadiliko hayo ya mwezi Agosti, bei za mafuta zimeshuka nchinzima kutokana na mwenendo wa bei katika soko la dunia:


Petroli: Imeshuka kwa TZS 92 kwa kila lita.

Dizeli: Imeshuka kwa TZS 204 kwa kila lita.

Mafuta ya Taa: Yameshuka kwa TZS 440 kwa kila lita.

View attachment 3643462View attachment 3643463


Inashangaza sana,

Kwenye kupanda bei kiwango kilikuwa kikubwa sana , yaani kutoka elfu 2 hadi elfu 4.

Kwenye kushuka sasa, kidogo kidogo sana, mwezi huu wanashusha kwa senti 2, kesho kwa shillingi 1....

Halafu kwa nini nchi kama Uganda bei ya mafuta kwao ni ndogo kuliko sisi? Upigaji.
 
Kupanda ni 1,000/- kushuka 92, 90 bado bei ipo juu,
Inabidi ukiwa na 10,000/- at least upate lita 3 za mafuta hapo itakua kweli yameshuka
 
Back
Top Bottom