EWURA yatangaza bei mpya za Mafuta kwa Mwezi June 2026

EWURA yatangaza bei mpya za Mafuta kwa Mwezi June 2026

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Hali ni mbaya kwa wamiliki wa Diesel.
===========
Mabadiliko ya bei za mafuta nchini kwa mwezi Juni 2026 yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na mzozo unaoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran ulioanza tarehe 28 Februari 2026.

Mashambulizi yaliyofanyika kwenye visima vya mafuta, maghala ya kuhifadhi mafuta na viwanda vya kusafisha mafuta, pamoja na kufungwa kwa Mlango wa Hormuz (Strait of Hormuz) ambao hupitisha takribani asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa duniani, yameathiri uzalishaji na usambazaji wa mafuta kutoka Mashariki ya Kati, ambako Tanzania hupata sehemu kubwa ya bidhaa zake za mafuta.

Hali hiyo pia imeongeza gharama za usafirishaji kutokana na upungufu wa meli za mizigo na kuongezeka kwa gharama za bima kwa meli zinazobeba mafuta.

Ongezeko la bei za mafuta ni changamoto ya kimataifa, na Tanzania kama sehemu ya dunia imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unaendelea kuwa wa uhakika huku ikidhibiti bei ili kupunguza athari za kiuchumi na kijamii.

Katika hatua hiyo, Serikali imetoa ruzuku ya Sh534.91 kwa lita moja ya dizeli ili kupunguza bei ya bidhaa hiyo muhimu inayotumika katika shughuli kubwa za kiuchumi kama uzalishaji viwandani, usafirishaji wa bidhaa na huduma za usafiri wa umma.

Kutokana na hali hiyo na mzozo unaoendelea ambao umeathiri miundombinu ya mafuta Mashariki ya Kati na kuhatarisha usalama wa upatikanaji wa mafuta duniani, wananchi wanashauriwa kutumia mafuta kwa uangalifu na kwa ufanisi zaidi.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (EWURA) imetangaza bei elekezi za juu za bidhaa za mafuta zitakazotumika Tanzania Bara kuanzia Jumatano, tarehe 3 Juni 2026 saa 12:01 asubuhi.

Kwa mwezi Juni 2026, bei za rejareja na jumla za bidhaa za mafuta katika miji ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zimewasilishwa katika Jedwali Na. 1.
IMG_8908.jpeg



IMG_8909.jpeg
IMG_8910.jpeg
IMG_8911.jpeg
IMG_8912.jpeg
IMG_8913.jpeg
 
Back
Top Bottom