EWURA yatangaza bei mpya za mafuta, Petrol yapanda, Dizeli imeshuka

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) imetoa bei mpya za mafuta ya dizeli na Petroli zitakazoanza kutumika kuanzia Novemba 4.

Kwa Dar es salaam Bei za rejareja ya Petroli imeongezeka kwa Tsh 25 kwa kila lita na bei ya Mafuta ya Taa imeongezeka kwa Tsh 12 kwa lita. Huku bei ya dizeli ikiwa imeshuka kwa Tsh 44 kwa lita.

Bei ya jumla kwa Dar kwa Petroli imepanda kwa Tsh 28.07 kwa lita, bei ya mafuta ya taa imeongezeka kwa Tsh 14.95 kwa lita huku bei ya dizeli ikiwa imepungua kwa Tsh 41.32 kwa lita.

EWURA imesema mabadiliko haya ya bei yanatokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia la mafuta.
 
Attachments

Safi sana sasa wanyonge tuna enjoy maana bei ya mafuta imekua ndogo kama ya huko Saudia.

Asante kwa awamu ya 6.
 
Tunaomba na "NAULI" ziongezwe ili wafanyabiashara wa mabasi wapate nafuu, mwendo kasi nauli iwekwe 1,000/=. Na bidhaa zote zipande kwasababu usafiri utakua juu (Mfano: Sukari ipande kutoka 2,500/= mpaka 3,000/=... Cement itoke 19,000/= mpaka 25,000/=... Sigara itoke 200/= mpaka 400/=).

Ili wale kenge waliokua wanapiga kelele kuunga juhudi za Kaisari kusema yupo kusaidia wanyonge, akili ziwasogee.

NB: Kuna tetesi mabeberu wanampango wa kuziomba nchi zinazotuuzia mafuta waache kutuuzia. Hapo lazima bei ya Petrol/Diesel ipande mpaka 15,000/= kwa lita moja.
 
Ushaambiwa mabadiliko ya bei yanatokana na mabadiliko kwenye soko la dunia.

Awamu ya 6 inahusikaje hapa?
Awamu ya 6 inamiliki visima vya mafuta vingi tu kule arabuni ndio maana wameweza kushusha bei ya mafuta mkuu

TUNATEKELEZA
 
Tunaomba na "NAULI" ziongezwe ili wafanyabiashara wa mabasi wapate nafuu, mwendo kasi nauli iwekwe 1,000/=. Na bidhaa zote zipande kwasababu usafiri utakua juu (Mfano: Sukari ipande kutoka 2,500/= mpaka 3,000/=... Cement itoke 19,000/= mpaka 25,000/=... Sigara itoke 200/= mpaka 400/=).

Ili wale kenge waliokua wanapiga kelele kuunga juhudi za Kaisari kusema yupo kusaidia wanyonge, akili ziwasogee.
Na internet bando la 1GB walipandishe liwe Tsh.15,000 ili tuweze kupata kodi nyingi tujenge sgr kila wilaya na Ma Stigler's ya kutosha.
 
Wale wanaccm wenzangu tutaendelea kununua Kwa bei Ile ya zamani hii bei mpya ni Kwa wapinzani Tu....tunawaomba ewura wapandishe bei kila mwez Ili wapinzani waache kutumia Magari Yao na waanze kutumia baiskel.
 
Safi sana sasa wanyonge tuna enjoy maana bei ya mafuta imekua ndogo kama ya huko Saudia.

Asante kwa awamu ya 6.
Bado tuko awamu ya tano, awamu siyo uchaguzi tu Bali hutokana na badiliko la rais mfano angeshinda lisu ndio tungekuwa awamu ya sita
 
Tunaomba na "NAULI" ziongezwe ili wafanyabiashara wa mabasi wapate nafuu, mwendo kasi nauli iwekwe 1,000/=. Na bidhaa zote zipande kwasababu usafiri utakua juu (Mfano: Sukari ipande kutoka 2,500/= mpaka 3,000/=... Cement itoke 19,000/= mpaka 25,000/=... Sigara itoke 200/= mpaka 400/=).

Ili wale kenge waliokua wanapiga kelele kuunga juhudi za Kaisari kusema yupo kusaidia wanyonge, akili ziwasogee.

NB: Kuna tetesi mabeberu wanampango wa kuziomba nchi zinazotuuzia mafuta waache kutuuzia. Hapo lazima bei ya Petrol/Diesel ipande mpaka 15,000/= kwa lita moja.
Cement kwetu tunanunua elf 22000 tangu january 2020 mpaka sasa
 
Wale wanaccm wenzangu tutaendelea kununua Kwa bei Ile ya zamani hii bei mpya ni Kwa wapinzani Tu....tunawaomba ewura wapandishe bei kila mwez Ili wapinzani waache kutumia Magari Yao na waanze kutumia baiskel.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom