Ewura yatangaza bei za mafuta mwezi Aprili, Dar Petroli yapanda hadi 3,037

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Bei ya mafuta imeendelea kuongezeka kwa miezi miwili mfululizo huku kwa watumiaji wa petroli wakilazimika kuzama zaidi mfukoni.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano Aprili 2, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).

Bei ya mafuta ya petroIi Aprili hii kwa mafuta yanayopitia bandari ya Dar es Salaam yatauzwa Sh3,037 kwa lita moja ambayo imeongezeka kutoka Sh2,996 Machi, huku dizeli ikipaa kutoka Sh2,885 Machi hadi Sh2,936 mwezi huu.

Na kwa yale yatakayopitia Tanga petroli itauzwa Sh3,083 ikitoka Sh3,042 Machi na dizeli ikipaa kutoka Sh Sh2,932 Machi hadi Sh2,982.

Pia, Petroli itakayopita katika bandari ya Mtwara lita moja itauzwa kwa Sh3,109 ikilinganishwa na Sh3,069 mwezi uliopita, huku dizeli ikiuzwa Sh3,008 mwezi huu ikilinganishwa na Sh2,958 ya Machi.
GneJ9g0WoAAe94V.jpeg
 
Attachments

View attachment 3290903
Kwa hiyo CCM wameanza kupunguza deni la mama la Trillion 97.35 kupitia mafuta. Wananchi hohehahe wanazidi kukamuliwa bila sababu.
 
Na bado
Ngoja tumsikie Trump leo na Liberation Day yake
Huku nje kila kitu kimepanda kuanzia jana
Na joto la maisha tumeanza kulihisi
Ni mwendo wa kutafuta hela tu hakuna kulia
Tunajifunza mpaka kupaka Rangi ili kuongeza kipato 😄
 
Chura awezi rizika kuwaibia watanganyika nao ni mabwege mpk December itafika mpk elfu 5 kwa lita. Yy CHURA anachakupoteza anawaza uchaguzi TU. Na sio kuwatumikia watanganyika.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Bei hii hata uwe na IST unajifanya haili mafuta... Buku tatu inakuhusu... Labda uende kuweka mtungi wa gesi..
 
Back
Top Bottom