Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kati ya Julai 2023 hadi Juni 2024 imefanikiwa kutatua migogoro 258 ya malalamiko kuhusiana na sekta inazozisimamia.
Hayo yameelezwa na Meneja Uhusiano na Mahusiano wa EWURA, Titus Kaguo wakati wa mafunzo ya udhibiti wa huduma za mamlaka hiyo kwa Chama cha Wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA), tarehe 13 Desemba, 2024 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Kaguo amesema katika malalamiko hayo 83 (33%) ni ya ankara, 47 (17%) ni kuhusu maunganisho ya huduma, 18 (7%) ni trespass, 34 (13%) yanahusu huduma kwa mteja (customer service), 13 (5%) ni fidia, 1 (1%) inayohusiana uharibifu wa mali, 10 (4%) ni kuhusiana na majanga ya moto na 4 (2%) inahusiana na usalama wa afya, mali na mazingira.
Akizungumzia sekta ya maji amesema kuwa mamlaka za maji hazitakiwi kuondoa huduma kwa mteja wakati wa wikendi, huku akisisitiza kuwa mita za maji zinatakiwa kusomwa akiwepo mteja husika na si vinginevyo.
Pia ameongeza kuwa katika kudhibiti sekta ya maji, mamlaka hiyo hutoa leseni kwa mamlaka za maji nchini, uhamasisha uvunaji wa maji pamoja na kupokea na kuchambua taarifa za utendaji, ambapo EWURA hutumia taarifa hizo kuelekeza ama kushauri ili kuboresha huduma.
Aidha, Kaguo amewataka Watanzania kupitia mkataba wa huduma kwa mteja ili inapotokea changamoto iliyosababishwa na mamlaka inazosimamia waweze kulipwa fidia, kulingana na mkataba wa huduma kwa mteja na kanuni za ubora wa huduma.
Kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha Sheria ya EWURA pamoja na majukumu mengine, mamlaka hiyo inalojukumu la kusimamia utatuzi wa malalamiko na migogoro miongoni mwa watumiaji huduma na watoa huduma.