EWURA yazitaka mamlaka za maji nchini kutoa taarifa sahihi za huduma ya maji na usafi wa mazingira

EWURA yazitaka mamlaka za maji nchini kutoa taarifa sahihi za huduma ya maji na usafi wa mazingira

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
2,010
Reaction score
4,179
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.

8C76F43E-180D-4F34-872B-1BE48D972872.jpeg

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato, amezitaka Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini kuhakikisha zinatoa taarifa sahihi za huduma ya maji na usafi wa mazingira kwa wananchi ili kushamirisha upatikanaji wa huduma endelevu kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Mhandisi Lumato ametoa maelekezo hayo leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22.

Mhandisi Lumato ameeleza kuwa tathmini iliyofanywa na EWURA imebaini kuwapo mamlaka za maji ambazo zimeendelea kuwasilisha taarifa zenye mapungufu kwenye kukidhi viwango vya huduma, uchakavu, ufanisi wa makusanyo wa maduhuli, muda wa upatikanaji wa huduma, ubora wa maji pamoja na idadi ya wananchi wanaopata huduma, hali hii inakwamisha kufanya tathmini ya hali halisi ya utendaji na upatikanaji huduma.

“Nitoe wito kwa mamlaka zote za maji kuhakikisha zinafanya masahihisho kwenye taarifa zenye mapungufu ili ziweze kutoa hali halisi ambayo mwisho wa siku itasaidia katika kupima utendaji na ufanisi wa huduma wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira” amefafanua Mhandisi Lumato

Kwa upande wake Mwakilishi wa katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Adam Ishara,amezitaka Mamlaka hizo kujitahidi kutekeleza wajibu wake kwa kutoa takwimu sahihi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa huku akisisitiza kuwa, Wizara ipo tayari kutoa miongozo na ushirikiano unaohitajika muda wowote.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira,ambaye ni Meneja Ufundi wa Maji na Usafi wa Mazingaira EWURA, Mhandisi Titus Safari,amesema kuwa mchakato wa maandalizi ya ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji ni shirikishi hivyo kila mamlaka itumie kikao hicho kuthibitisha usahihi wa taarifa zake.

WATENDAJI kutoka Mamlaka 25 za Majisafi na Usafi wa Mazingira za miji mikuu ya mikoa na mamlaka 7 za miradi ya kitaifa wamehudhuria kikao kazi hicho kinachofanyika makao makuu ya EWURA jijini Dodoma.

DF179BBF-CDC7-460B-B133-D22620C38B29.jpeg

65D6CADC-3BA1-4DB4-85DF-5E24E3B19446.jpeg

SEHEMU ya Watendaji kutoka Mamlaka za Maji wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,(hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.

ECA53194-AC52-44F0-8320-9F276081F667.jpeg

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato (katikati) akifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.Kulia ni Mhandisi Adam Ishara kutoka Wizara ya Maji na kushoto Meneja Ufundi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA Mhandisi Titus Safari.

DA7A4086-5A7A-4290-972A-7C397AD5061E.jpeg

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Idara ya Maji na Usafi wa Mazingira mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.

4380CA9B-360F-4C5B-B33F-DCADADBF7DA4.jpeg

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mamlaka za maji na Miradi ya kitaifa mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.
 
Nilitegemea ni kikao cha yeye kutumbuliwa kwa sababu maji hayapo na hakuna hatua za haraka zilizochokuliwa kutunusuru na kero hii.

Ni aibu Daslam kurudia maisha ya mwaka 2008 ya kero za maji na supply ya maji ya chumvi kwa maboza na mikokoteni ndio yalioshika hatamu kila kona ya jiji na watawala wanakula shushu tu kama hakuna tatizo lolote.
 
Nilitegemea ni kikao cha yeye kutumbuliwa kwa sababu maji hayapo na hakuna hatua za haraka zilizochokuliwa kutunusuru na kero hii.

Ni aibu Daslam kurudia maisha ya mwaka 2008 ya kero za maji na supply ya maji ya chumvi kwa maboza na mikokoteni ndio yalioshika hatamu kila kona ya jiji na watawala wanakula shushu tu kama hakuna tatizo lolote.
Extrovert angali kuwa hai bwana mwenda zake hayo yasingekuwepo shida ni kwamba tumefanywa kama kichwa cha mwenda wazimu na hata ukichunguza utabaki unajiuliza kwanini alipokuwepo hizi adha kama Maji,Umeme,Usafi wa Mazingira na Miundombinu zote zilikua zikizingatiwa sana na utendaji wake ulikuwa wa hali ya juu kweli sasa ni nini kimetokea kwani hata ule utaratibu wa usafi mwisho wa mwezi umekufa..
 
Extrovert angali kuwa hai bwana mwenda zake hayo yasingekuwepo shida ni kwamba tumefanywa kama kichwa cha mwenda wazimu na hata ukichunguza utabaki unajiuliza kwanini alipokuwepo hizi adha kama Maji,Umeme,Usafi wa Mazingira na Miundombinu zote zilikua zikizingatiwa sana na utendaji wake ulikuwa wa hali ya juu kweli sasa ni nini kimetokea kwani hata ule utaratibu wa usafi mwisho wa mwezi umekufa..
Kulikuwa na sababu kubwa ya kumu assasinate yule mzee, waxenge ni wengi sana kwenye system. Laiti kama....would kill all muthafuckaz with my bare hands!

Mtu anakufa ghafla, slogan inageuzwa from "working only" to "Resuming the work"! A year after kila kitu kiko kisengele nyuma tu. Wananchi sote tuko in the deathrow and nobody gives a flying fucck!
 
Kulikuwa na sababu kubwa ya kuuwawa yule mzee, waxenge ni wengi sana kwenye system. Laiti kama....
Tuliache tu hili iwe imebaki story yani nikiutafakari huu msemo wa NABII HAKUBALIKI KWAO nagubikwa na maswali mengi sana ambayo hayataweza pata majibu kamwe.
 
Inatia hasira sana kmmmk yani dah,
Once nilishawahi kujiuliza wale wenzetu wanawezaje kujitoa mhanga kwa ajili ya wengi kwani huwa mtu anakua amechoshwa na maisha kwa hali gani hadi kuweza kufikia hatua hiyo by then now I realize within a situation like this kweli mtu anaweza akapokea kibunda na kufanya hayo maangamizi bila Shaka!
 
Once nilishawahi kujiuliza wale wenzetu wanawezaje kujitoa mhanga kwa ajili ya wengi kwani huwa mtu anakua amechoshwa na maisha kwa hali gani hadi kuweza kufikia hatua hiyo by then now I realize within a situation like this kweli mtu anaweza akapokea kibunda na kufanya hayo maangamizi bila Shaka!
Inawezekana bruh.
 
Inawezekana bruh.
Yah! Lkn sio kwa sisi wabongo mzee yani ishu ya maji ndio mtu ajitoe mhanga wakati hiyo hela ya kumpa huyo mtu ajitoe mhanga unaweza geuza ya mradi binafsi unachimba visima vya kutosha kisha unapiga hela zaidi Thahahahaaaa!!!
 
Kuna mchezo mmoja wazungu wanaota 'hot potato' ,viongozi ndio wanatuchezea.litakayemdondokea kuja kujifanya anatatua kero za wananchi,,kichwa chake ndio kitaenda. Huyo bwana kamrushia dawasa,nategemea dawasa atahemewa na waziri wa maji soon...
 
Huwa natamani kujua maji yanalipwa shilingi ngapi kwa Lita..
Au wanaitumia mfumo gani kuhesabu Ankara za maji
 
Back
Top Bottom