EX anataka kuwa mchepuko wangu

EX anataka kuwa mchepuko wangu

Ndara Mbovu

Senior Member
Joined
Feb 28, 2017
Posts
155
Reaction score
83
Habarini za siku wana JF

Nilikuwa na mchumba wangu kwa miaka 3, Tuliachana kwa kuwa nilimpa hela ya mkopo akafanyie biashara yeye akachukua hela kwenda kufanyia matumizi yake binafsi kama kukarabati nyumba ya baba yake na nyingine akafanyia biashara, kwa kifupi alinidhurumu pesa yangu.

Alidai ameniacha na amenidhurumu hizo pesa kwa kuwa nina mtoto naye, hivyo pesa itamsaidia kumjengea maisha mtoto. Sababu ya kufanya hivyo ni kwa kuwa nilimsaliti.

Baadaye mtoto wetu alifariki, nikamwambia turudiane mana nilijihisi hasara sana mana pesa ile nilifikiri itamsaidia na mwanangu na sikuona maumivu kudhurumiwa, sasa mwanangu amefariki.

Nikaona basi turudiane nimpe ujauzito mwingine, nilitaka tuishi pamoja, akakataa na kusema anataka kwenda kusoma. Mi sikuona haja ya kuendelea naye. Nikaanzisha mahusiano na mwanamke mwingine ambaye alikuwa mpenzi wangu wa zamani ambaye tulipendana sana.

Ex wangu aliposikia nataka kuoa alikuja kwangu na kuniambia sasa hatoenda shule atabaki tuishi pamoja kama kusoma atasoma open university, nampenda sana huyu binti, nilimjibu haiwezekani kurudiana, alilia sana na kujuta sana.

Sasa nimeoa mwanamke ambaye nampenda naye ananipenda na wala sitaki kumkosa, yule ex wangu bado ananililia anadai ananipenda sana anataka awe hawala yangu na nizae naye.

Naogopa mke wangu akija kujua na pia naona hasara ex wangu anamiliki vitu vingi vya kwangu na biashara, karibuni kuchangia wadau.
 
Mweleze mkeo. Mwambie kuwa unampenda huo mwingine.

Mwambie anataka umfanye mchepuko ila kwa vile hiyo ni dhambi wewe unataka kumuoa kama mke wa pili.

Halafu njoo tuendelee na ushauri baada ya jibu lake.
 
Sasa nimeoa mwanamke ambaye nampenda naye ananipenda na wala sitaki kumkosa,

yule ex wangu bado ananililia anadai ananipenda sana anataka awe hawala yangu na nizae nae .

Naogopa mke wangu akija kujua na pia naona hasara ex wangu anamiliki vitu vingi vya kwangu na biashara ,karibuni kuchangia wadau.
Sasa ndio manini haya?

Had hapo inaonesha umeisha hamua kurudiana na huyo ex wako
 
Habarini za siku wana jf

Nilikuwa na mchumba wangu kwa miaka 3,
Tuliachana kwa kuwa nilimpa ela ya mkopo akafanyie biashara yeye akachukua ela kwenda kufanyia matumizi yake binafsi kama kukarabati nyumba

Ngoja wahuni wenzio watakupa kuchangia
 
Usipokua makini utavunja ndoa yako. Achana na huyo mchepuko ukikaza fuvu hapa ndugu yatakufika mazito.
 
Back
Top Bottom