Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Upendo haugawanyiki lazima kuna unayempenda zaidi kati yao...(utaamua mwenyewe ni yupi)Habarini za siku wana jf
Nilikuwa na mchumba wangu kwa miaka 3,
Tuliachana kwa kuwa nilimpa ela ya mkopo akafanyie biashara yeye akachukua ela kwenda kufanyia matumizi yake binafsi kama kukarabati nyumba ya baba yake na nyingine akafanyia biashara , kwa kifupi alinidhurumu pesa yangu,
Alidai ameniacha na amenidhurumu hzo pesa kwa kuwa nina mtoto nae, hvyo pesa itamsaidia kumjengea maisha mtoto.
Sababu ya kufanya hvyo ni kwa kuwa nilimsaliti .
Baadae mtoto wetu Alifariki , nikamwambia turudiane mana nilijihisi hasara sana mana pesa ile nilifikiri itamsaidia na mwanangu na sikuona maumivu kudhurumiwa, sasa mwanangu amefariki. Nikaona basi turudiane nimpe ujauzito mwingine, nilitaka tuishi pamoja, akakataa na kusema anataka kwenda kusoma .Mi sikuona haja ya kuendelea nae .
Nikaanzisha mahusiano na mwanamke mwingine ambaye alikuwa mpenzi wangu wazamani ambaye tulipendana sana.
Ex wangu aliposikia nataka kuoa alikuja kwangu na kuniambia sasa hatoenda shule atabaki tuishi pamoja kama kusoma atasoma open university ,nampenda sana uyu binti ,nilimjibu haiwezekani kurudiana, alilia sana na kujuta sana,
Sasa nimeoa mwanamke ambaye nampenda naye ananipenda na wala sitaki kumkosa,yule ex wangu bado ananililia anadai ananipenda sana anataka awe hawala yangu na nizae nae .
Naogopa mke wangu akija kujua na pia naona hasara ex wangu anamiliki vitu vingi vya kwangu na biashara ,karibuni kuchangia wadau.
Ila kama utaamua kulamba matapishi basi kuwa tayari kubeba gharama zitakazo ambatana na maamuzi yako.