Ex-GF kajitangaza anao, napata kero vibaya

acha longolongo nenda kapime utupe majibu. Ndo tukushauri
SIMPLE AND CLEAR, na ukukuta hauna na wewe jiunge na kwenye matangazo ya wauza CONDOM kuhusu umuhimu wa kuvaa condom kuwa uliwahi kuwa na GF ambaye baadaye alipima na kujitangaza kuwa ana ngoma wewe uko safi so jamani nawashauri wenzangu fungeni mikanda wakati wote wa safariiiii
 

jamani nyie mbona mnaona kama rahisi sana kiivyo hili janga letu wote mwacheni mpaka hapo atakapokuwa tayari mwenyewe kucheki afya yake
 
jamani nyie mbona mnaona kama rahisi sana kiivyo hili janga letu wote mwacheni mpaka hapo atakapokuwa tayari mwenyewe kucheki afya yake

Wakati atakapokuwa tayari ni upi? Akianza kukohoa kwa TB au atakapolala kitandani kimoja baada ya CD4 kushuka sana? Na kwanini aogope kama kweli alikuwa anatumia rough rider? Wakati wa kupima ni SASA if you knoo woram seyyiiing.
 
Mkuu,bila kurefusha hadithi, nenda kapime, vinginevyo utaishi kwa wasiwasi na utajitia maradhi ya fikra bure(stress)

Kaka Kwanza nakupa pole sana kwa masahibu yaliyokupata.
Ukitaka kuepukana na dhihaka au namna nyingine ya kunyanyapaliwa nakushauri kapime habari,eti ulikuwa haufanyi ngono hazita saidia kitu.

Ishi kwa matumaini, nenda kapima na uchukue majibu yako!

yaani hapo tu ni kuonyesha kuwa condom haziaminiki ki hivyo

sasa mkuu utakuja kutupa majibu hapa (walau yakiwa mazuri?)
 
Pole sana Mtu B,inabidi ukapime ili ujue status yako.vipimo ndo vitasema ukweli.
 

Ninajibu hiyo bolded kama ulivyouliza. Mimi naelewa ngono zembe kuwa ni ile inayoweza kusababisha mimba na/au magonjwa ya zinaa. Na ninaelewa kuwa mtu akitumia kondomu kwa usahihi na kwa kila tendo la ngono, basi hiyo ni ngono salama (kinyume cha ngono zembe). Nimekuwa nikifanya hivyo katika ngono zote nilizoshiriki, isipokuwa moja tu niliyokuwa nikifanyishwa nikiwa mtoto wa miaka 10 (18 years ago) ndiyo niliyokwenda kavu, na ndipo nilipojifunzia ngono.

Kwa uelewa wangu VVU vinaingia kwa urahisi kwenye via vya uzazi, na hasa kama kuna michubuko. Sijawahi kupata mchubuko huo maana siku zote nakuwa nimevaa kondomu.

Siwezi kumwomba msamaha huyo dada maana kufanya hivyo ni sawa na self-implication kwa kosa lisilokuwa langu. Hakuna baina yetu mwenye uhakika kama kabla hatujakutana nae alikuwa nayo hiyo HIV au la. Siko tayari kujinyanyapaa kwa kitu kisicho na ushahidi.

Kuhusu kumsifu huyo uliyesema, niwie radhi mshikaji maana mie na hizo dini za kukopa kwa watu wa middle east tuko mbalimbali. Wanaohusika nae watamsifu tu hamna noma.
 
yaani hapo tu ni kuonyesha kuwa condom haziaminiki ki hivyo

sasa mkuu utakuja kutupa majibu hapa (walau yakiwa mazuri?)

Nimedhamiria majibu nitaleta hapa, yawe mazuri au mabaya. Lakini ninawahakikishia sitoyatoa kwa forum ya wanaonifahamu kihalisi, maana huu unyanyapaa unatisha, naipenda amani yangu.
 

mambo mengine bana! kama kula denda inasababisha hiv basi wengi tuu
watakuwa wameathirika. nielewavyo mimi ni kwamba virusi viletavyo hiv
kama vitakuwepo kwenye mate basi ni kiasi kidogo sana ambacho hakiwezi sababisha maambukizi. aidha, ili mtu aambukizwe kupitia mate inabidi wahusika wawe na michubuko kinywani kisha hayo mate wabadilishana kwa dozi kubwa sana.
 

hiyo haikuwa ngono bali mchezo, hivyo usikonde lol
 
mimi nakushauri kafanye vipimo vitatu kutoka kwa madaktari tofauti alafu hao wataokusumbua kwamba unao waonesha hayo majibu. ikiwezekana chukua namba za simu za hao madaktari hili kama bado hawakuamini waweze kuwapigia simu hao madaktari ku-confirm.
 
Mtu B
Kwanza nakupa pole kwa situation unayopitia ndugu yangu
Pili naomba niwaambie hao wote wanaokutumia message na kukupigia simu za kukunyoshea vidole washindwe na kulegea
Tatu naomba kukwambia kuwa uwe na amani moyoni mwako kwa kuwa hili litapita na hakika utakuja kutuambia kuwa wewe ni salama salimini. Wote tunafanya makosa bwana hata kama sio kwenye ngono lakini kwenye mambo mengine.
Ila Bahati Mbaya sana nimesoma sehemu kuwa huamini katika Yesu Kristo na kusema kuwa ni dini za kukopa Mashariki ya Mbali lakini kwa kuwa mimi namwamini na kumtegemea nitakuombea uwe salama ndugu yangu hata utakapoenda kupima.
Mwisho wadau waJF binafsi kama kijana nimejifunza mengi kwenye thread hii na michango yenu, hope you too
 
Wakati atakapokuwa tayari ni upi? Akianza kukohoa kwa TB au atakapolala kitandani kimoja baada ya CD4 kushuka sana? Na kwanini aogope kama kweli alikuwa anatumia rough rider? Wakati wa kupima ni SASA if you knoo woram seyyiiing.

chrispin we acha Binamu usiseme haya mambo yasikie kwa mwenzio
Mtu B mwaya me am zea for u
count on my support please
 
chrispin we acha Binamu usiseme haya mambo yasikie kwa mwenzio
Mtu B mwaya me am zea for u
count on my support please

Yalishawahi kukukumba? Mi yalishawahi na nikasepa. Ishukuriwe kondom. Thats why namshauri AKAPIME ASAP!
 
Ishi kwa matumaini, nenda kapima na uchukue majibu yako!
unadhani ni kirahisi jinsi hiyo?,lazima mtu awe well prepared,Takwimu zinaonyesha watu wengi wanakimbia majibu baada ya kupima.Yataka moyo kwa kweli.
 
unadhani ni kirahisi jinsi hiyo?,lazima mtu awe well prepared,Takwimu zinaonyesha watu wengi wanakimbia majibu baada ya kupima.Yataka moyo kwa kweli.

Hahaha! You can say it again! Mchumba kwa takwimu bana! LOL!
 
 
Hahaha! You can say it again! Mchumba kwa takwimu bana! LOL!
Ndio wewe mwenyewe mshauri wangu ulinifundisha hayo ya takwimu.
Lakini hebu sema ukweli,unafikiri ni kirahisi?,mie pia huu wasiwasi nimewahi kuupata kama mara 2 hivi maishani mwangu,nakwambia ilikuwa balaa,nilikuwa nasikia kufakufa kila wakati yani sikuwa na raha.Kila nikisikia neno ukimwi au linalofanana na hilo iwe redioni au popote moyo unashituka ghafla na naondoka siendelei kusikiliza.Lakini badae niliokoka na hali ile ikaanza kuisha japo sio sana.lakini nilipata ujasiri wakupima.
 
yalishawahi kukukumba? Mi yalishawahi na nikasepa. Ishukuriwe kondom. Thats why namshauri akapime asap!

hayajawahi ila nakumbuka mala ya kwanza nimeenda kupima sikuchukua majibu nikakata kona si kwamba nilikuwa nacheza faulo la hasha ila nilikuwa nawaza maybe sindano au ile ppe haikuwa salama or nk nk
 

Mi nilikuwa mwoga kupita kiasi. Ila siku nilipomwona brother anakaribia kufa kwa kupungukiwa na damu, damu ikawa nzito zaidi, nikajitolea kupima. Ilikuwa siku ya kutisha. Tangu hapo, sijawahi kuogopa kupima. Infakti reagents ziko pale home, sometimes najipimaga mwenyewe!! Watu watafikiri natania ujue, ila wewe najua utanielewa.

Hiyo red hiyo! Mchumba imani yako bado haijakaa sawa. Funga na kuomba zaidi. Watu wa namna hiyo hawana woga mbele ya chochote chini ya mbingu.
 

Maneno mazuri sana haya ndugu yangu, nimefarijika nakushukuru mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…